Mgombea wa
Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana ameibuka mshindi wa uchaguzi
mdogo wa udiwani katika kata ya Mianzini uliofanyika jana kwa kupata kura 1283,
huku Mgombea wa Cuf akipata kura 494, Chadema wakiambulia kura 315 na ADC
walipata kura 26, NRA kura 9 na Mgombea wa NCCR Mageuzi akiambulia kura 1.
Bawji amemzidi mshindi wa pili kwa zaidi ya nusu ya kura.
Mara baada ya matokeo kutangazwa na tume kupitia kwa
Afisa Mtendaji wa Kata, Wanachama wa CCM waliletewa matokeo yale na kusomwa na
Mkurugenzi wa uchaguzi wao ambaye ni Katibu kata wa Mianzini wa CCM, Abdallah
Kihuku mbele ya hadhara ya Wana CCM waliofurika katika ofisi za kata.
Mshindi mteule wa Udiwani wa Kata ya Mianzini,
Athman Bawji Mbwana akiongea machache kwa Wana CCM mara baada ya kutawazwa kuwa
mshindi. Bawji anaziba nafasi iliyokuwa wazi kufuatia kifo cha diwani wa kata
hiyo.....
Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, Ramadhan Madabida
akiwashukuru wana CCM kwa umoja na mapambano ya dhati yaliyopelekea ushindi wa
CCM. Huu ndio uchaguzi wake wa kwanza tangu awe Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es
Salaam na ni uchaguzi mdogo wa pekee wa udiwani kwa Mkoa wa Dar Es salaam
Katibu wa Mkoa wa CCM, Abdillah Mihewa naye pia akitoa yake ya moyoni.
Katibu
wa Wilaya ya Temeke wa CCM, Ndg Robert Kihaka akiwashukuru Wana CCM kwa
uvumilivu wao na jitihada zao zilizozaa matunda mema.
Mida ya jioni, tayari wana CCM walishaanza heke heka za kushangilia ushindi.
Mawakala wa CCM wakiwasili katika ofisi za kata kwa kuwasilisha taarifa za matokeo ya uchaguzi kwa chama
Mjumbe
wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Emmanuel John akiwasili toka
kuwakusanya mawakala wa CCm kwenye vituo vyao vya kupigia kura.
Wana CCM walifurika katika ofisi za kata ya Mianzini wakishangilia ushindi. Ilikuwa ni raha tupu.
No comments:
Post a Comment