Mbunge wa Monduli, ambaye pia ni
waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha
UDOM waliotoka shule za sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani
Dodoma kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.
Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye
hafla hiyo Juni 25, 2013.
Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wanafunzi wa Chuo Kikuu ch DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika
hapo wakitokea zile shule za makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa
Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea urais
2015 muda utakapowadia.
Pia wameahidi kujichangisha fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo
endapo italazimika.
Kauli hiyo ya kwanza kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo ndani ya
siasa, ilitolewa Jumatatu usiku nyumbani kwa Lowasa mjini Dodoma, wakati kundi nla
wanafunzi hao walipofika kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia ikiwa ni
matunda ya shule hizo, ambazo muasisi wake ni mbunge huyo wa Monduli.
“Mimi ninayofuraha kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana
ninayesoma elimu ya juu, baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya sekondari
kupitia shule za kata pale Kiluvya Dar es Salaam” anasema Hamida Salum ambaye
kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo UDOM.
“Wewe ni jembe, kama uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa
kipindi kifupi cha miaka 2, ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo
utakuwa rais wan chi hii” mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza, Clementina
Ophoro alisema, kwenye salamu za mwanafunzi mmoja mmoja wakati wa utoaji
shukrani kwa Lowasa.
Lowasa wakati akiwa waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu
ya n ne ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za
kata kote nchini, ili kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela,
walioishindwa kendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba
wa madarasa.
Kwa sasa shule hizo zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo
kuwa hazina walimu wa kutosha na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo vyumba
vya maabara.
“Mimi ninawashangaa watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa
vile hazina walimu na vifaa. Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu hupaswi
kukwepa changamoto za maisha” alisema mwanafunzi mwingine Victor Mafuru pia wa
mwaka wa kwanza.
Wanafunzi hao wa UDOM waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua
kuanzisha umoja wao kote nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha kila
mwanafunzi wa mtu masikini anapata elimu.
Kwa kuanzia wanafunzi hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye
shule za umma, wawapo likizo baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.
Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na Naibu Waziri wa kazi na
ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu
wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa
shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa
shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha
Mapinduzi, zimeweza an galau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga
na vyuo vikuu. Habari hii ni kwa hisani ya Father Kidevu Blog.
No comments:
Post a Comment