Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA
Cha Alliance For Democratic Change (ADC), kimesema kuwa sasa vyama vya CCM na
CUF vimeanza kupoteza umaarufu wake katika siasa za Tanzania, hivyo kuna siku
vitapotea kusipojulikana na kuwaacha wengine wakifanya vizuri.
Mwenyekiti wa ADC, Said Miraaj katikati akizungumza na waandishi wa habari juu ya siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa Uchaguzi Mdogo jimbo la Chambani, uliomalizika kwa CUF kushinda na kutetea jimbo lao. Kulia ni Doyo Hassan Doyo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa ADC, Said Miraaj, alisema kuwa
hilo limedhidhirika pia katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chambani, ambapo CUF
na mgombea wao Yussuf Salim Hussein walipata ushindi wa jumla ya kura 2708.
Alisema
ingawa wao wameshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 112 nyuma ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), waliyopata kura 202, huku washindi ambao ni Chama Cha Wananchi
CUF kikipata kura 2708, wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
wakipata kura 12, ila njia yao ni nzuri katika kuelekea wao kufanya vizuri
kuliko vyama vingine vya siasa.
"Pemba
kuja chama na kufanya vizuri ni ngumu mno, ndio maana hata ndugu zetu Chadema
wao licha ya kufanya vizuri katika siasa za Tanzania Bara, lakini kule walipata
kura 12 tu.
"Sisi
kama ADC tunaamini tutafanya vizuri zaidi, hasa kama wapiga kura wetu
wataendelea kutuamini na kutuunga mkono, ukizingatia sisi ndio wasemaji wakuu
wa watu wa Zanzibar, baada ya ule muundo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa,”
alisema.
Aidha
ACD kimemjia juu Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kulitaka Jeshi la Polisi
kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu watakaokaidi amri zao, katika
matukio ya kijamii na kisiasa.
Kauli
hiyo si ya kwanza kutolewa na watu mbalimbali, wakiwamo wanasiasa tangu Pinda
alipotoa kauli hiyo, akichukulia mfano wa mlipuko wa bomu jijini Arusha na
jinsi wananchi walivyoshindwa kutii amri halali ya jeshi la Polisi na kuzua
mgogoro mzito, huku wakisaidiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
No comments:
Post a Comment