Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ALHAMISI ya jana, itakuwa chungu kwa sanaa na wasanii baada
ya kutokea vifo viwili vya wasanii, akiwapo mwimbaji wa Hip Hop, Langa Kileo na
mcheza filamu wa Bongo Movie, Hassan Kihiyo.
Marehemu Langa Kileo enzi za uhai wake
Vifo vyote hivyo vilitokea jana, baada ya kulazwa katika
Hospitali walipokuwa wakitibiwa na kusababisha vifo vyao na kuleta majonzi
makubwa katika sanaa Tanzania.
Marehemu Ngwair aliyezikwa mkoani Morogoro wiki iliyopita na kuzua balaa kubwa kwa mashabiki wake.
Marehemu Kihiyo anatarajiwa kuzikwa leo jioni katika
makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni, jijini Dar es Salaam, wakati Langa yeye
atazikwa Jumatatu, katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Msanii wa maigizo Kash aliyezikwa mapema wiki hii.
Wadau mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti juu ya mwendelezo
wa vifo hivyo, ukizingatia kuwa vimetokea siku chache baada ya kuzikwa Albert
Mangweha ‘Ngwair’ na mwanadada Kash msanii wa maigizo aliyezikwa mapema wiki
hii.
Msanii nguli na mtunzi wa filamu Tanzania, Muddy Kimindu
Kulinyangwa, aliiambia Handeni Kwetu kuwa Kihiyo ni miongoni mwa wasanii wenye
mchango mkubwa katika sanaa.
Msemaji wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha,
aliimbia Handeni Kwetu jana jioni kuwa chanzo cha msiba wa Langa kitajulikana
baada ya ripoti kutolewa na daktari wake, ingawa habari zilizobuka pia zinasema
msanii huyo wa Hip Hop alikuwa na malaria kali.
Ratiba juu ya msiba wa Langa imetoka, huku ukiwa nyumbani
kwao Mikocheni, ambapo Jumatatu utazikwa baada ya tukio la kumuaga
likikamilika.
Hata hivyo, wapo waliozidisha makali juu ya kifo cha Langa
kwa kukihusisha moja kwa moja na matumizi mabaya ya dawa za kulevya, ambapo
msanii huyo alikuwa akitumia kabla ya kuumanisha umma kuwa ameacha ulaji huo wa
dawa za kulevya.
Langa ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania waliokuwa
wamejiingiza katika vitendo vibaya vya uvutaji huo wa dawa za kulevya, jambo
lillosababisha pia umaarufu wao na uwezo wao kisanaa kuchuka kama sio kwisha
kabisa.
Langa aliibuka katika kundi la Wakilisha, likiwa na wasanii
watatu, Sara, Witness nay eye mwenyewe, ambapo walichomoza baada ya kushinda
shindano la Coca Cola Pop Stars nchini Afrika Kusini.
Nyimbo zilizoimbwa na kufanya vizuri ni pamoja na Swanglish,
Matawi ya Juu, pamoja na nyimbo nyingi alizoshirikishwa ukiwapo ule wa Chagua
Moja wa Fid Q.
No comments:
Post a Comment