Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
MWILI wa msanii
Albert Mangwea, umezuiwa na Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini wakiwa na
lengo la kushiriki kumuaga, hivyo kulazimisha kupanguliwa kumleta nchini kesho
(leo) na badala yake marehemu atawasili kesho Jumapili.
Marehemu Ngwea, enzi za uhai wake
Aidha, wadau
mbalimbali wameendelea kushiriki kuchangia msiba wa marehemu Ngwea, wakiwamo
Kampuni ya Clouds Media Group, sambamba na Studio za Bongo Records chini ya
P-Funk Majani na Push Mobile ambao wote kwa pamoja wamechangia Milioni tano
kila mmoja.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba,
alisema kuwa wamepata taarifa kutoka Afrika Kusini kuwa mwili huo sasa
utawasili kesho Jumapili ya Juni mbili badala ya Jumamosi ya Juni Mosi kama
ilivyotangazwa awali.
Alisema kuwa
Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini nao wametaka kuweka utaratibu wa
kuuaga mwili huo kabla ya kuletwa Tanzania, hivyo imelazisha kupangua ratiba ya
kuwasili kwa mwili huo.
Naye Mkurugenzi wa
Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutaba, alisema kuwa wameamua
kushirikiana kwa karibu na wadau wote katika kufanikisha kuuleta mwili huo hapa
nchini.
Akizungumza na
Mtanzania jana jijini Dar es Salaam, Ruge alisema Watanzania wote wameguswa na
msiba wa msanii Mangwea kutokana na mchango wake kwenye sanaa.
Alisema kuwa
kinachoangaliwa kwa sasa ni kukaa pamoja na wadau kwa ajili ya kufanikisha
kuletwa kwa mwili wa marehemu Ngwea aliyefia nchini Afrika Kusini na
kuhuzunisha wadau wengi.
“Clouds
tumeshirikiana na wadau wote hasa wa Kamati ya Mazishi ambayo ipo chini ya
mwenyekiti wake, Kenneth Mangwea ambaye ni kaka wa marehemu kwa ajili ya
kufanikisha suala hilo,” alisemaa.
BASATA
yamlilia Mangwea
Nalo
Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa
msanii Mangwea, aliyefia nchini Afrika Kusini kwenye shughuli zake za kimuziki.
“Baraza
limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Ngwea
ambaye mchango wake unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo aliloliacha
ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii,” alisema
taarifa hiyo iliyotumwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Lebejo.”
Alisema
Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha
linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na
mpendwa wetu.
Ngwea atakumbukwa kwa
mchango wake katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya, akishiriki kuandaa nyimbo
zilizopokelewa kwa shangwe, ukiwapo wimbo wa Gheto Langu.
No comments:
Post a Comment