Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MWENYEKITI
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi,
amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendeka rasimu ya
katiba.
Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Mwenyekiti wa UVCCM Kilimanjaro akiongoza maandamano kuelekea katika ukumbi wa CCM mkoa ambapo ndipo ilikofanyikia mkutano mkubwa wa UVCCM jana |
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la
Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa
kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali
tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa
muungano.
Viongozi waandamizi wa CCM mkoani Kilimanajro katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa |
“Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni
mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali
tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu
huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana
tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu
wa sasa,"
“Vijana
tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa, taaluma zetu
ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wetu kwani
ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na usalama wan chi yetu, tuepuke
kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi haitatawalika,” amesema
Hata
hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na
maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana
na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.
|
“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine
vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha
kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi
ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la
wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya
akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani
ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa
kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
|
Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo,
ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto
wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo
hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa
wanafunzi hao.
|
“Mikopo
ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima tutairudisha
lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo kwa watoto wa
masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea kuzungushwa na kuwekewa
masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,” alisema..
|
No comments:
Post a Comment