FAINALI za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,zinafanyika mkoani Tanga
siku ya Jumapili Tarehe 19-5-2013katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga. Fainali
hizo za tano za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005,
zitajumuisha jumla ya warembo 30 kutoka mikoa yote ya Tanzania, na vyuo vikuu
watapanda jukwaani kuwania taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/13.
Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni mkataba wenye thamani ya sh.90,
000,000/=,ambao unajumuisha skolashipu ya kusoma kozi ya Diploma katika chuo
cha Dar es Salaam City Collage, safari za kushiriki mashindano ya Dunia,ziara
za Tanzania Great Safari and Tour 2013, kugharamiwa usafiri wakati wa shughuli
za kutekeleza majukumu yake ya ushindi,na shilingi 5,000,000/= baada ya
kutumikia taji lake wakati wa kukabidhi kwa mshindi wa msimu ujao.
Aidha mshindi wa pili hadi wa tano, kila mmoja kila mmoja atajipatia
mkataba wenye thamani ya shilingi 58,000,000/=, ambao pia unajumuisha skolaship
za kusoma chuo cha Dar Es Salaam City Collage na safari za kushiriki mashindano
ya kimataifa nay a dunia, pia ushiriki wa safari za Tanzania Greet Safari and
Tour 2013 na kugharamiwa usafiri wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya
ushindi. Washiriki walio bakia watajipatia tuzo mbalimbali za heshima, za
utalii, utamaduni, jamii, uchumi, mitindo, ,wanyama
pori,misitu,mazingira,utalii wa ndani,utalii wa kitamaduni,jinsia,utalii wa
michezo,utalii wa mikutano,elimu ya jamii,afya ya jamii, urembo na maliasili.
Mashindano ya Dunia ambayo washindi hao watashiriki ni Miss Tourism World
2013, Miss Tourism United Nation 2013, Miss Tourism University World 2013, Miss
Heritage World 2013, Miss United Nation 2013,Miss Freedom Of The World 2013,na
Miss Globe International 2013.
Burudani katika fainali za mwaka huu ,zitakazo fanyika kitaifa mkoani
tanga jumapili tarehe 19-5-2013, ni pamoja na Bendi ya Msondo Ngoma, Mwana
mziki wa kimataifa Che Mundu Gwao, Ngoma za asili na vichekesho kutoka kundi la
Majuto Arts Group linalo ongozwa na mwigizaji mahili na mkongwe Mzee
Majuto,sarakasi na muziki wa kizazi kipya yani bongo fleva.Maandalizi
yamekamilika, na hali ya kambi ni shwari huku washiriki wote wakiwa katika hali
ya kujiamini, kila mmoja akijigamba kupeleka jaji mkoani kwake mwaka huu.
Katika shindano la mwaka huu, katika ukumbi wa CCM Mkwakwani, wabunge
,madiwani,wakuu wa wilaya,na viongozi wa vyama na serikali wamealikwa
kuhudhuria. Mkuu wa mkoa wa Tanga Mheshimiwa Chiku Galawa atakuwa mgeni rasmi
katika fainaali hizo za kihistoria kufanyika mkoani Tanga.
Tumepeleka fainali za jumapili katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, ili
kutoa fulsa kwa wakazi wa kada zote kushudia fainali hizo, kwani shindano hili
ni kwa ajili ya watanzania wote bila kujali utofauti wao wa vipato wala
umri,ndo mana viingilio ni vya beii ya chini sana, ambapo shindano
litaanza mchana wa saa 7 hadi usiku wa manane. Viingilio watoto itakuwa
2000/=, wakubwa mzunguko itakuwa shilingi 5,000/=, viti maalum shilingi
20,000/= na viti vya kawaida ni shilingi 10,000/=.
No comments:
Post a Comment