Waandishi wa Habari wakiwa kazini
LEO ni siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Kwasababu hiyo,
Handeni Kwetu blog inawatakia kila la kheri waandishi wote duniani. Mikono yao
ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa lolote duniani. Naamini siku kama ya leo
wataitumia kutafakari changamoto zao.
Waandishi wa habari za michezo, Onesmo Kapinga akifuatilia jambo kwenye kompyuta na Zaituni Kibwana.
Ingawa waandishi kioo
cha jamii, lakini nao kama binadamu wa kawaida kuna mahali wanakosea kwa sababu
moja ama nyingine. Pia, licha ya umuhimu wao huo, lakini wengi wao wamekuwa
wakiishi maisha ya kawaida.
Baadhi yao wananufaika na majina ambayo hata hivyo hayana
tija kwao. Hata hivyo, bado haitakuwa sababu ya kutoheshimu mchango wao. Ni
wakati wao sasa kuona kuwa Taifa linahiwahitaji kwa namna moja ama nyingine.
Muandishi wa Habari za Kimataifa wa Gazeti la Mtanzania, Joseph Hiza kulia akiwa na Markus Mpangala, wakifurajia jambo.
Kushoto kwao ni Mhariri wa Makala wa gazeti hilo, Hamisa Maganga akiwa kazini.
Hii ni faida kubwa kwao. Changamoto katika jambo lolote ni
matokeo ya kawaida, hivyo bila kukata tama, waandishi wanapaswa kuungana na
kufanya kazi kwa nguvu moja. Pia wapo waandishi ambao kwa mtazamo hasi,
wanaojiona wao ni bora kuliko wenzao.
Hii inazalisha chuki miongoni mwao na kuwafanya wasiwe
wamoja katika kukaa na kutafakari maisha yao kwa ujumla. Huu ni wakati wa
kufunga mkanda. Bila hivyo, miaka nenda rudi, waandishi wa habari watakuwa
daraja la maisha bora yaw engine huku wao wakifa njaa.
Handeni Kwetu blog inawatakia kheri waandishi wote ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment