Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) limempongeza
bondia maarufu wa kitanzania Francis Cheka kwa juhudi zake za kuwa bondia mzuri
mwenye viwango vya kimataifa katika uzito wa Super Middleweight.
Francis
Cheka aliweza kutetea mkanda
wake wa IBF Africa uzito wa Super Middle baada ya kumshinda kwa KO
bondia Thomas Mashali aka “Simba asiyefugika” tarehe 1 Mei, 2013
katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.
Francis Cheka
IBF inachukua fursa ya kumpongeza Francis Cheka baada ya ushindi huo
ambao umedhihirisha kuwa yeye kweli ni bingwa wa bara la Afrika. Francis Cheka atarudiana na bondia wa
Malawi Chimwemwe Chiotcha mwezi
wa Agusti katika mpambano la
kutetea mkanda wake.
Mpambano wao wa marudiano utafanyika katika
jiji la Blantyre nchini
Malawi na tayari majadiliano
ya mpambano huo yanaendelea vizuri. Kampuni ya “Mawenzi Boxing Promotion” ya nchini Malawi chini ya bwana Stephen
Mawezni ndiyoitakayoandaa mpambano huo.
Pambano hili linakuja baada ya wadau kadhaa wa
ngumi kuomba mabondia hao warudiane walipoonyesha ujuzi mkubwa na ushindani
katika mpambano wao Desemba 26
mwaka jana katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeidi jijini Arusha siku ya Boxing
Day.
Baada ya mpambano huo, IBF itampatia Francis Cheka nafasi ya kugombea
mkanda wa IBF wa Kimataifa (IBF
International Super Middleweight) na mabondia wa Ulaya au Marekani. Hii ni kudhihirisha kuwa Francis Cheka hana tena mpinzanai
nchini Tanzania na kumpambanisha na mabondia wa kitanzania ni kumpotezea muda
na uwezekano wake wa kutengeneza jina na pesa.
Wakati
huo huo bondia Thomas Mashali bado ni bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBF)
katika uzito wa Middle kwani
mkanda wake haukuwa kati ya mikanda iliyogombewa kwenye mpambano uliomalizika
Mei mosi.
No comments:
Post a Comment