Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umetamba kuwa watani zao wa jadi Simba,
wataishia kunawa kama wana ndoto au lengo la kuchukua mchezaji wao yoyote
wanayemuhitaji abaki kwenye kikosi chao.
Baraka Kizuguto, Msemaji wa Yanga
Yanga na Simba wapo kwenye vita ya kuwasainisha nyota wao, huku
Yanga wakifanikiwa kupata saini ya Mrisho Ngassa kutoka Simba, hiku juzi Haruna
Niyonzima naye akitia saini ya kubaki jangwani kwa misimu mwili zaidi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga,
Baraka Kizuguto, alisema kuwa hakuna nyota wanayemtaka akasajiliwa na Simba,
hivyo benchi la ufundi na usajili linafanya kazi muda wote.
Alisema anaamini kila mchezaji imara na hodari mwenye uwezo
atabaki Yanga pamoja na kuongeza wengine kulingana na mahitaji ya benchi lao la
ufundi, linaloongozwa na Ernest Brandit.
“Tunasikia mengi kutoka kwa watani wetu, ila juu ya kupata saini
za mchezaji wetu kutoka Yanga, labda awe ahitajiki kulingana na mtazamo wa
benchi la ufundi, maana hawatapata hiyo nafasi.
“Tumeshafanikiwa kuipataa saini ya Niyonzima, kinachofuata sasa ni
kuwaangalia wengine, akiwamo Hamis Kiiza, Nurdin Bakari, ambao nao mikataba yao
imekwisha na Yanga inawahitaji,” alisema Kizuguto.
Yanga inaingia kwenye vita vya usajili huku ikijivunia kunyakua
ubingwa wa Ligi ya Tanzania Bara, sambamba na kumtandika mtani wake wa jadi,
Simba kwa mabao 2-0 na kuwafurahisha mashabiki wao.
No comments:
Post a Comment