Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda pichani, ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili
kupisha kamati ya uongozi ya Bunge iendelee kukutana ili kutoa maamuzi na tamko
kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki
dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi
wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.
Pia mjadala wa makadirio ya
mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini umesimamishwa kwa muda mpaka
ufumbuzi wa tatizo la vurugu hizo utakapopatiwa suluhisho.
Kesho bajeti ya makadirio ya
mapato na matumizi ya Afrika Mashariki itajadiliwa.
Taarifa ya serikali bungeni
kuhusu vurugu zilizotokea Mtwarailisomwa na Nchimbi badala ya PM, Chanzo kikuu cha vurugu ni
kupinga gesi kusafirishwa kutoka Mtwara hadi Dar. Vurugu zilianza kwa
kusambazwa vipeperushi vya kuhamasishana kufanya vurugu.
Nyumba ya Mbunge imechomwa,
ofisi za CCM kata, Nyumba na ofisi mbalimbali watu 91 wamekatwa, hali hiyo
imedhibitiwa jeshi la ulinzi limeenda kwa ombi la RC ambapo wakiwa njiani
kuelekea huko askari 4 wamefariki kwa ajali ya gari.
Nawapongeza askari waliofanya
kazi katika mazingira magumu kurudisha hali ya amani.
No comments:
Post a Comment