https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, May 31, 2013

Kampuni ya Clouds Media Group yakiri kujitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kutoka Afrika Kusini hadi Tanzania kwa mazishi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Clouds FM, imejitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kwa ajili ya kuutoa Afrika Kusini hadi Tanzania kwa ajili ya kuzikwa, ukiwa ni utaratibu unaoonyesha kuwa wadau wote wameamua kushirikiana katika suala hili.
Barua inayoonyesha walioanza kuchangia msiba wa Ngwea
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, alithibitisha kuchukua uamuzi huo kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya nyota huyo wa Bongo Fleva.
                                 Marehemu Albert Mangwea
Taarifa za Kampuni hiyo kusaidia zilianza kuenea tangu juzi, baada ya Kamati ya Mazishi kushindwa kutaja makampuni, taasisi na watu walioanza kuchangia kwenye msiba huo.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
"Tumeamua kwa mikono miwili kushiriki katika msiba huu wa ndugu yetu Mangwea,” alisema kwa ufupi.

Ngwea amepangwa kuletwa Tanzania kesho Jumamosi na kuagwa Jumapili, kabla ya kupelekwa mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...