|
|
|
Sehemu la Daraja la Rau,
lililoko katika manispaa ya Moshi, Mkoani Kiliamnajro lililokataliwa na
Viopngozi wa CCM wilaya ya Moshi katika ziara ya kukagua miradi ya manispaa
Moshi ili kujiridhisha kama miradi inayoendeshwa na Manispaa hiyo ianendena
na kiwango kinachotakiwa.
|
|
|
|
Na Mwandishi Wetu Moshi
CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Moshi, imelikataa daraja la manispaa
iliyojengwa katika kata ya Rau mbokomu lililojengwa kwa kutumia fedha za
serikali kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ujenzi wake.
Wakizungumza baada ya kukagua daraja hilo, ambalo pamoja na ujenzi wake
kutokamilika na kukabidhiwa kwa wananchi, Viongozi wa CCM wilayani hapa ambao
walikuwa katika ziara maalum ya kukagua miradi ya serakili iliyojengwa katika
manispaa hiyo, walisema inasikitisha kuona kazi muhimu kama ujenzi wa daraja
likitekelezwa kizembe.
Viongozi hao kutoka katika Kamati ya Siadsa ya Halmashauri kuu CCM wilaya ya
na Sekreteriet ya Halmashauri kuu ya CCM wakiongozwa na Mjumbe wa Mkutano mkuu
CCM Taifa, Aggrey Marealle, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi, Elizabeth Minden
a Katibu wa CCM wilaya, Aluu Segamba wamelikataa daraja hilo kutokana na
kutoridhishwa na kiwango chake.
Wakiwa wameongozana na Mkadiriaji wa Gharama za ujenzi wa Manispaa ,
Mhandisi Charles Huka na Msaidizi wa Mchumi wa Manispaa, Evera Lyimo. Viongozi
hao walisema hata kiasi cha fedha cha sh. Milioni 102, kilichotengwa kwa ajili
ya ujenzi wa daraja hilo lililoanza kubomoka hata kabla ya ujenzi wake
kukamilika ni kidogo mno ikilinganishwa na ukubwa wa kazi.
Akizungumzia tamko lao, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi,
Aluu Segamba alisema kimsingi wao kama chama tawala, hawajaridhika na kiwango
cha ujenzi wa daraja hilo huku akiwataka wananchi kutopitisha magari yao katika
daraja hilo kwa usalama wao na kuongeza kuwa ujenzi huo unatakiwa urudiwe upya.
Alisema kuwa kilichofanyika katika daraja hilo ni uhuni mtupu na kuongeza
kuwa hawatakubali kuona fehda za umma zikiteketea ovyo kutokana na uzembe wa
watu wachache.
“Kimsingi hili daraja hatujaridhika na kiwango cha ujenzi wake, huu ni uhuni
na kamwe kama chama tawala hatuwezi kukaa kimya huku fedha za umma zikitafunwa
kizembe, utajengaje daraja kwa kutumia milioni 102? Tunawaomba wananchi
wasipitishe magari hapa hadi litengezwe katika kiwango kinachoridhisha,”alisema
Segamba.
Naye Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa, Aggrey Marealle alisema kuwa baada ya
kufanya ziara hiyo wanatarajia watakaa na kujadili kwa kina na kasha kutuma
mtaalamu wao katika miradi yote waliyokagua na kasha watatuma mapendekezo yote
kwa wizara ya ujenzi.
Hata hivyo Mkadiriaji wa gharama wa ujenzi wa manispaa, Charles Huka,
ambaye katika ziara hiyo alimwakilisha Mhandisi wa Manispaa,
Alipoulizwa kuhusu ujenzi wa daraja hilo, alisema kuwa muda wa mkataba wa
mkandarasi haujakamilika na kimsingi wao wanaridhishwa na ujenzi huo.
Huka alisema kuwa kilichotokea ni sehemu ya udongo kumeguka huku akiongeza
kuwa wanachokisubiri ni muda wa mkataba wa mkandarasi huyo kukamilika ndipo
watakapotoa maelezo wa nini kimefanyika ila kwa sasa wanaridhika na kiwango cha
ujenzi na wana imani na mkandarasi wao.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa eneo hilo pamoja na kupongeza manispaa
kwa kuwahjengea daraja katika eneo hilo, wameonesha wazi wasiwasi juu usalama
wao na kuliomba serikali kuhakikisha daraja hilo halileti madhara kwao.
Wakizungumza na gazeti hili, Mchungaji Frank Machange, ambaye ni mratibu wa
mazingira katikiamkaisa KKKT jimbo la Moshi na mwananchi Emmanuel Erick
walisema kitendo cha kujengewa daraja katika eneo hilo ni la kupongeza lakini
kuna hali ya hatari kutokana na daraja kuanza kumeguka.
Miradi mingine iliyokaguliwa na Viongozi wa CCM katika ziara hiyo ni, Ujenzi
wa Nyumba za walimu katika shule ya msingi Msandaka, shule ya sekondari mji
mpya, Maabara ya Shule ya secondari Rau, madarasa manne Moshi Technical,
Majengo ya Hospitali ya Pasua na Sehemu ya barabara ya Mwamedi Sadiki,
inayounganisha kata ya Boma mbuzi na Majengo mapya.
Akitoa maelezo ya barabara hiyo, Mwenyekiti wa Mtaa, kata ya Majengo Mapya,
Beatrice Kimambo alisema kuwa barabara hiyo ambayo alidai baada ya kuona ujenzi
wake haukidhi viwango yeye pamoja na viongozi wenzake katika ODC walimuuliza
diwani wao lakini walijibiwa kwamba swala la barabara hiyo haliwahusu.
Wanaolalamikia katika ubadhirifu wa ujenzi wa mifereji katika barabara hilo
ni Meya wa Moshi ambaye ndiye diwani wa kata ya Boma mbuzi, Japhary Michael na
Diwani wa Majengo Mapya, Charles Makarakara.
Kimambo aliwaeleza viongozi hao kwamba katika kufuatilia gharama
zilizotumika katika ujenzi wa kingo za miferuji katika barabara hiyo ambayo
mwaka mmoja tuu tangu ijengwe imeanza kubomoka, waliambiwa na diwani wao kuwa
ni bilioni moja.
|
No comments:
Post a Comment