Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
LIGI
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu
(2012/2013) inafikia tamati kesho (Mei 18 mwaka huu) kwa timu zote 14
kupambana katika viwanja saba tofauti.
Itakuwa balaa
Mechi
zote zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Ni jukumu la kamishna wa
mechi husika kuhakikisha mchezo unaanza katika muda uliopangwa,
vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi
Kuu ya Vodacom toleo la 2012.
Yanga
ambayo tayari imeshatwaa ubingwa itakuwa mgeni wa Simba katika mechi
namba 180 itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo mwamuzi
atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro na Kamishna ni Emmanuel Kavenga wa
Mbeya.
Mgambo
Shooting vs African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mwamuzi ni Amon
Paul wa Mara wakati Kamishna ni Ally Mkomwa kutoka Pwani), JKT Ruvu vs
Mtibwa Sugar (Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Mwamuzi ni Israel
Mujuni wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Salum Kikwamba kutoka
Kilimanjaro).
Tanzania
Prisons vs Kagera Sugar (Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mwamuzi ni Ibrahim
Kidiwa wa Tanga wakati Kamishna ni John Kiteve kutoka Iringa), Oljoro
JKT vs Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha. Mwamuzi ni
Athuman Lazi wa Morogoro wakati Kamishna ni Juma Mgunda kutoka Tanga).
Uwanja
wa Jamhuri, mjini Morogoro utatumika kwa mechi kati ya Polisi Morogoro
na Coastal Union ya Tanga ambapo Mwamuzi atakuwa Said Ndege wa Dar es
Salaam wakati Kamishna ni Hakim Byemba kutoka Dodoma. Toto Africans
itacheza na Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
ambapo mwamuzi ni Geoffrey Tumaini kutoka Dar es Salaam na Kamishna ni
Josephat Magazi wa Singida.
No comments:
Post a Comment