Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU mbili za Soya na Bungu
Kibaoni wilayani Korogwe mkoani Tanga zimepenya katika hatua ya kwanza ya
michuano ya Gambo iliyoanzishwa na Mrisho Gambo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya Korogwe, Mrisho Gambo
Timu hizo sasa zinasubiri
kuingia hatua ya robo fainali kwa kusubiri timu nyingine kwenye makundi manne yaliyowekwa
kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mshindi halali anapatikana kwa kupitia michuano
hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu,
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka wilayani Korogwe, Peter Juma, alisema kuwa ligi
yao inaendelea vyema kwa timu za Soya na Bungu Kibaoni kupenya hatua ya kwanza.
Alisema kuwa anaamini kuwa timu
nyingine zitaonyesha uwezo wa juu katika kushiriki michuano hiyo yenye mguso
katika wilaya ya Korogwe iliyoandaliwa na DC Gambo.
“Sisi kama wasimamizi wa
michuano hii ya Gambo Cup tunaamini kuwa lengo ni kuona mashindano yetu
yanafanya vyema na kukuza mchezo wa soka wilayani hapa.
“Timu za Soya na Bungu kibaoni
zitasubiri timu za makundi mengine na baadaye kushiriki hatua ya robo fainali
kwa mtindo wa makundi ambapo ni utaratibu uliowekwa kwa ajili ya kufanikisha
mashindano haya ya Gambo Cup wilayani Korogwe,” alisema Juma.
Mashindano hayo ya Gambo Cup
yalizinduliwa na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete, ambaye
ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
No comments:
Post a Comment