Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaa,
CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
kinatarajia kuendesha kozi ya makocha pamoja na waamuzi ili kusaidia kuinua
kiwango cha mchezo huo.
Msemaji wa DRFA, Mohamed Mharizo
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, kikao cha Kamati ya Ufundi, kilichoketi Mei 11 mwaka
huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, chini ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Joseph
Kanakamfumu, alisema kozi ya ualimu wa mpira wa miguu ngazi ya cheti
(Inter-Mediate), ambayo imekuwa kwenye mahitaji makubwa, itaanza Juni 3 hadi 28
mwaka huu.
Kozi itakuwa kwa siku 10, tunatarajia kupata washiriki
watakaofikia 60, iwapo idadi hiyo itafikia na kuzidi, kutakuwa na awamu mbili
za wanafunzi ambao kisheria darasa linatakiwa kuwa na wanafunzi 35 hadi 40.
Watu wataanza kujiandikisha kuanzia Mei 15 hadi
26 na awamu ya kwanza ya kozi itaanza Juni 3 hadi 14 na ya pili itaanza
Juni 17 hadi 28.
Ada ya ushiriki itakuwa Sh 50,000 na itahusisha gharama ya
kuchukulia fomu 5,000 na zilizobaki ni gharama ya cheti, kitambulisho pamoja na
chakula cha mchana.
Kwa
upande wa kozi ya waamuzi itaanza Septemba 3 hadi 9 mwaka huu na ada itakuwa Sh
25, 000.
Fomu
zitapatikana katika ofisi za Mikoa ya kisoka, TEFA, IDFA,KIFA na DRFA na kozi
zote zitafanyika kwenye ukumbi huo wa Harbours Club.
Kamati
hiyo imepanga kukutana Mei 19 kwenye Ukumbi huo wa Harbours Club saa tatu
asubuhi na viongozi wote wa timu za wanawake kutathimini michango yao kwa
ukuzaji wa soka la Wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam.
Wajumbe waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa
Kamati ya Mashindano ya DRFA, Kennedy Mwaisabula, Jovin Ndimbo (Mwenyekiti
Kamati ya Waamuzi), Benny Kisaka (Mwenyekiti Kamati ya Soka la Wanawake),
Abdallah Mitole (Mjumbe kamati ya waamuzi), Sijali Juma (Mjumbe kamati ya waamuzi),
Richard Mbuya (Mjumbe kamati ya Soka la Wanawake) na Dk. Maneno Tamba (Mjumbe
Kamati ya Soka la Wanawake).
No comments:
Post a Comment