https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, May 10, 2013

Wakati watu wakimsimanga kila siku, Ruge Mutahaba aula Simba SC



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, ameula katika klabu ya Simba, baada ya kuteuliwa kuwa mjumbe kwenye Kamati ya Mpango Mkakati Strategic Plan.
Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group ambaye ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Simba.

Mbali na Ruge, wadau wengine wakubwa wameingizwa kwenye kamati hiyo kwa ajili ya kuiweka klabu hiyo kwenye nafasi za juu kwa kutumia mawazo ya watu hao katika kamati, huku uteuzi huo ukitarajiwa kuwa bakora ya kuwaadhibu wenye kukosoa mwenendo wa mdau huyo, ambaye baadhi ya watu kwenye sanaa wamekuwa wakimsema kila wakati kuwa anachangia maisha magumu ya wasanii.

Kuteuliwa kwa Ruge kwenye Kamati hiyo inaonyesha kuwa mchango wa mtu huyo ni mkubwa kiasi cha kuhitajiwa kila mahali, yakiwamo mambo ya burudani na michezo.

Taarifa iliyosambazwa na Katibu Mkuu wa Simba, ambaye naye yupo kwenye kamati hiyo, Evodius Mutalawa, ilisema kuwa klabu imeingia makubaliano na Open University Consultancy Bureau (Hapa itafaamika kama “OCB”) kwa ajili ya kuandaa mpango mkakati wa klabu (strategic plan).

Mchakato huo unaanza mara moja na OCB wameshaandaa timu yao inayoongozwa na makamu mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwette ambapo ili kufanikisha hilo imebidi kuunda kamati ya marejeo ya Simba SC (Referral committee) ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuiongoza OCB :-

1. Kuhusu makundi/watu/maeneo yatakayotumiwa kufanya utafiti.
2. Kunyambulisha kitaalamu nguvu, mianya na maeneo ya maboresho ya mfumo mzima wa Simba SC (SWOT analysis)

3. Kupitia mpango mkakati ukishaandaliwa baada ya kukusanya maoni ya wanachama, wadau na mashabiki wa klabu kabla ya kuupeleka katika kamati ya utendaji kwa kupitishwa ili ukapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama.

Katika kikao cha kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika tarehe 8/5/2013 Referal Committee ya Simba Sports Club iliyochaguliwa ni:- Joseph Itang’are,
2. Swedy Mkwabi
3. Francis Waya
4. Ramesh Patel
5. Evance Aveva
6. Mulamu Ng’hambi
7. Salim Mhene
8. Mtemi Ramadhani
9. Moses Basena
10. Henry Tandau
11. Omary Gumbo
12. Michael Wambura
13. Glory Nghayomah
14. Crensencius Magori
15. Honest Njau
16. Ruge Mutahaba
17. Evodius Mtawala
18. Dr Mwafyenga

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...