Na Mwandishi Wetu, Mtwara
KUTOKANA na machafuko
yanayoendelea mjini Mtwara, wananchi zaidi ya 200 wamedaiwa kukimbilia kijijini
Naliendele ili kupumzika kwa maswahibu yanayoendelea katika mji huo, chanzo
kikiwa ni kugombania gesi isisafirishwe.
Picha na maktaba yetu.
Kwa siku tatu sasa mji wa
Mtwara umefurika askari polisi na jeshi kwa ajili ya kulinda usalama wa
wananchi kutokana na mgogoro huo na kulazimisha kupigwa kwa mabomu na watu
kadhaa kupoteza maisha yao.
Mwandishi wa Handeni Kwetu,
aliyopo mjini Mtwara alisema kuwa wananchi wengi wameamua kuuhama mji huo
kwasababu ya kuhofia usalama wao.
“Kumekuwa na ongezeko kubwa la
uchomaji wa nyumba za wananchi pamoja na wizi unaoendelea kuwaacha wananchi
kwenye wakati mgumu mno, hivyo wengi wao wameamua kukimbilia sehemu nyingine,”
alisema.
Kutokana na askari wengi
kumwaga mjini Mtwara, pilika pilika zimetulia, ingawa ni sehemu chache
zilizosikika milipuko, ukiwapo mtaa wa Msimbati, ambako jingo la Marine Park
lililipuliwa.
No comments:
Post a Comment