Na Mwandishi Wetu, Iringa
HABARI kutoka mkoani Iringa zinasema kuwa abiria
watano waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Taqwa lenye namba za
usajili T 273 CDR kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Malawi wamekufa papo hapo
na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea katika eneo la
Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mmoja
kati ya mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Dkt Matatala alisema kuwa ajali
hiyo imetokea mida ya saa 11 jioni wakati basi hilo likitokea Dar es Salaam
kwenda nchini Malawi.
Alisema
kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T 104 DZZ ambalo
lilikuwa likitokea Makambako kuelekea Iringa,lori lililokuwa likijaribu
kulipita lori lenye namba za usajili T 227 AVC na kushindwa kupita na kuishia
kugongana uso kwa uso na basi hilo ambalo pia lilikuwa likija kwa mwendo wa
kasi.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imetokea katikati ya
mji wa Nyololo ambapo ni jirani kabisa na eneo lenye matuta ya kuzuia magari
kwenda kwa mwendo kasi.
Alisema
kuwa hadi majira ya saa 12.45 jioni maiti tano zilikuwa zimetolewa katika basi
hilo la Taqwa na kuwa jitihada za wasamaria wema kutoa maiti na majeruhi katika
eneo hilo zimeendelea kufanyika.
Mbali
ya maiti hizo pia alisema jumla ya majeruhi 20 waliokolewa na kukimbizwa katika
Hospitali ya wilaya ya Mufindi kwa matibabu zaidi. Dkt Matatala alisema kuwa
katika tukio hilo wananchi wameweza kuimarisha ulinzi zaidi katika eneo hilo
ikiwa ni pamoja na kulinda mali za majeruhi na abiria waliopoteza maisha yao
kwa ajili hiyo.
No comments:
Post a Comment