Moses alisema tayari maandalizi
yameshaanza na mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo wote
wameshaingia kambini kujifua na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni
ya pili tangu yaanzishwe yatakuwa ni ya aina yake.
“Maandalizi yameshaanza, warembo
wote wapo kambini hapa katika ukumbi wa Aventure, kutoa burudani atakuwepo mtu
mzima Prince Dully Sykes, kila kitu kinakwenda sawa na tunategemea kushuhudia
kitu tofauti na yale ya mwaka jana,” alisema Komba.
Kuhusu swala la udhamini alisema
bado hilo ni tatizo huku wadhamini wakuu Redds na kampuni ya panone kwa
kujitolea kudhamini mashindano hayo. Akitangaza viingilio katika mashindano ya
mwaka huu, Komba alisema kuwa kwa viti vya dhahabu viingilio vitakuwa sh.
50,000, viti vya V.I.P vitakuwa ni sh. 30,000 na viingilio vya kawaida ni sh.
15,000.
Kwa upande baadhi ya washiriki wa
Redds Miss Moshi, wakizungumza na Gazeti hili katika kambi ya mazoezi, Jacky
Mushi, Winlady Mushi, Aichi Edwin na Rayness White walisema kuwa wabnatarajia
kutumia uzoefu watakaoupata kutoka katika mashindano hayo kulitumikia jamii
hasa wale waishio katika mazingira magumu.
Mashindano ya Redds Miss Moshi
2013 yatakayofanyika katika ukumbi wa Aventure, yanadhaminiwa na Redds, Panone
na Baba G na Zoom Net Printers ambapo kwa upande wa burudani alisema atakuwepo
msanii mkongwe wa kizazi kipya Dully Sykes akisindikizwa na wasanii wengine
kutoka Moshi.
No comments:
Post a Comment