Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi nchini
ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, imerudi tena katika Ukumbi wake
wa zamani wa Kijiji cha Makumbusho baada ya kuacha ukumbi huo kwa kipindi cha
miezi mitatu na kuwasononesha wadau wao.
Wazee wa Ngwasuma
Awali bendi hiyo ilikuwa
ikifanya shoo katika ukumbi huo, lakini kulitokea kutoelewana na vijana hao
kuamua kuacha kufanya shoo hapo, jambo ambalo kwa sasa limemalizika.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa FM Academia, Kelvin Mkinga, alisema
sasa vijana wao watatoa shoo Kijiji cha Makumbusho kila Jumamosi, kama kawaida
yao.
Alisema anaamini kurudi tena kwenye
ukumbi huo ni sehemu ya kuwaburudisha mashabiki wao waliokuwa wakihudhuria shoo
yao na kupata vitu adimu kutoka kwa vijana wao.
"Tulisimama kwa miezi kadhaa
kufanya shoo zetu Kijiji cha Makumbusho, lakini sasa tumerejea na Ngwasuma
wataendelea na ratiba yao ya zamani ya kila Jumamosi na kuburudika kwa pamoja.
"Utaratibu huo utaanza wiki hii
kuhakikisha kuwa vijana wanafanya makamuzi ya aina yake ili kuonyesha kuwa wao
ni vinara na Kijiji cha Makumbusho ni mahala pazuri kwa burudani zao,” alisema
Mkinga.
Wiki iliyopita Wazee wa
Ngwasuma walirejea kutoka kwenye ziara zao za mikoani walipotoa burudani za
aina yake, wakianzia mkoani Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Mbeya na Ruvuma.
No comments:
Post a Comment