Namba za Mchango wa Msiba ni 0754 074323 au 0658 074324.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMATI ya Mazishi ya msanii Albert Mangwea aliyefia nchini Afrika
Kusini, imewataka Watanzania wote kuungana juu ya kufanikisha kuuleta mwili wa
msanii huyo na kufanikiwa kuuweka kwenye nyumba ya milele.
Hayo yamesemwa leo mchana jijini Dar es Salaam na Msemaji wa
Kamati hiyo, Adam Juma, ambaye pia ameshirikiana na Shirikisho la Muziki
Tanzania, chini ya uongozi wake Addo Novemba.
Juma alisema kuwa gharama ni kubwa mno kuuleta mwili huo, hivyo
wadau na taasisi kwa pamoja washirikiane ili kuhakikisha kuwa msanii huyo
analetwa na kuzikwa mkoani Morogoro.
Naye Novemba alisema kuwa kwa kawaida gharama za msiba huo ni
kubwa, maana wamepanga waulete Jumamosi na kulala Hospitali ya Taifa Muhimbili,
huku Jumapili wakitarajia kuuaga kwenye Uwanja wa Leaders Club, jijini Dar es
Salaam, ambapo baada ya hapo wataupeleka Morogoro kwa ajili ya maziko.
Kuna vitu vingi vilivyopangwa ambavyo vyote vinahitaji gharama,
hivyo hatuwezi kukataa msaada wa mtu yoyote yule, maana ana haki kama binadamu
au Mtanzania,” alisema Novemba.
Hata hivyo, jana kwa mahesabu ya haraka haraka, Novemba aliweka
wazi kuwa zaidi ya Milioni 30 zinahitajika kwa ajili ya kufanikisha uletwaji wa
marehemu na maziko yake.
Kamati ya Mazishi imemjulisha wasanii mbalimbali, akiwamo Noorah,
TID, Profesa Jay, P-Funk, pamoja na kaka wa marehemu, Kenneth Mangwea.
Kwa yoyote anayetaka kuchangia alichokuwa nacho kwa ajili ya
kufanikisha msiba huo anatakiwa achangie kwa namba 0754 074323 au 0658 074324.
Msiba wa Ngwea kwa sasa upo nyumbani kwa kaka yake, Mbezi Beach,
maeneo ya Goigo. Aidha, Kamati imetangaza kuwa habari zozte za ripoti za kifo
cha Ngwea zilizosambazwa jana sio za kweli, maana zimebuniwa na watu wanaotaka
kumchafua marehemu.
No comments:
Post a Comment