Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA), Almas Kassongo (kushoto), akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Abajalo, Abbas Ngau Sh 600, 000 ikiwa ni mchango wa chama hicho
kusaidia timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka
huu.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana Alhamisi (Mei
9) jioni kwenye ofisi za chama hicho, zilizopo makutano ya mtaa wa Mafia na
Bonde, ambapo Red Coast waliokuwa washindi wa kwanza walikabidhiwa Sh 700,
000, huku Abajalo wao wakizawadiwa Sh 600, 000 na Friends Rangers wakijipatia
Sh 500, 000.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed
Mharizo, lengo la timu hizo kukabidhiwa fedha hizo ni kuzihamasisha ili
ziweze kujiandaa na hatimaye kufuzu kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo, ndiye
alikabidhi fedha hizo kwa wawakilishi wa timu hizo huku akisema licha ya
kiasi hicho cha fedha kuwa kidogo, lakini itakuwa chachu ya kupata mafanikio.
Viongozi waliohudhuria makabidhiano hayo kutoka
DRFA ni Mkurugenzi wa Ufundi, Joseph Kanakamfumo, Afisa Tawala, Said
Pambalelo, Mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano, Daudi Kanuti na
Mweka Hazina Ally Hassani.
Wawakilishi wa timu ni Mwenyekiti wa Red Coast,
Jumanne Ayubu, Meneja wa Friends Rangers, Shaaban Marsila na Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji wa Abajalo, Abbasi Ngau.
Wakati huo huo, kamati ya ufundi ya DRFA kesho
Jumamosi Harbours Club Kurasini, itakutana na Viongozi wa soka la Wanawake
(TWFA), Viongozi wa soka la Vijana na Kamati ya Waamuzi ili kupanga utaratibu
wa ligi na pia kuandaa kozi ya makocha.
|
No comments:
Post a Comment