Rais Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUZINDUA
MIRADI YA UJENZI WA BARABARA YA DODOMA – IRINGA YENYE UREFU WA KM 260 (SEHEMU
ZA DODOMA – FUFU ESCARPMENT, FUFU ESCARPMENT – MIGORI NA MIGORI – IRINGA) KWA
KIWANGO CHA LAMI TAREHE 22 MEI, 2013
Wizara ya
Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba, leo Mei 22 Mei, 2013 Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa
mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara kama
ifuatavyo:-
1)
Tarehe 22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu
Escarpment (km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini.
2)
Tarehe 22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu
Escarpment – Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji cha
Migori Wilayani Iringa Vijijini.
Barabara ya
Iringa – Dodoma ni sehemu ya barabara muhimu ijulikanayo kama “Great North
Road” inayoanzia Capetown Afrika ya Kusini hadi Cairo, Misri kupitia Tanzania.
Nchini Tanzania inaunganisha Miji ya Tunduma (mpakani na Zambia), Mbeya,
Iringa, Dodoma, Arusha na Namanga (mpakani na Kenya).
Mradi huu
ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu
muhimu ya usafiri wa barabara na unalenga kupanua fursa za kiuchumi na
kibiashara kwa wananchi, na kati ya Tanzania na nchi jirani za Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kwa
njia hii, barabara itakuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Taarifa
hii imetolewa na
Balozi
Herbert E. Mrango
KATIBU
MKUU
WIZARA YA
UJENZI
No comments:
Post a Comment