WASANII
wengi wanatarajiwa kuhudhuria kwenye tukio la ‘Made in Tanzania’ lenye kauli
mbio ya ‘Twenzetu Dodoma’, linalotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi mjini Dodoma
na kuandaliwa na Kampuni ya Clouds Media Group.
Wema Sepetu, msanii wa Bongo Movie
Twenzetu
Dodoma ni mpango maalumu wa kuwakutanisha watu mbalimbali wakiwamo wasanii
ambao nao wataitumia siku hiyo kutafakari mafanikio yao kwa kuangalia fursa
wanazokutana nazo.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media
Group, Ruge Mutahaba alisema kuwa lengo la kushiriki kwenye program hiyo ni
kutafuta fursa ya kimaisha, kwa watu mbalimbali wakiwapo wasanii Tanzania.
Alisema
watu wengi wamekubali kushiriki kwenye siku hiyo ya Made in Tanzania, akiwapo
Selemani Msindi Afande Sele, Wema Sepetu na wengineo.
“Hii ni
siku nzuri kwa watu wote kuangalia namna gani tunaweza kutafuta fursa ya
kimaisha, wakiwapo wasanii ambao kila siku wamekuwa watu wa kulalamika kuwa
wanaibiwa haki zao.
“Watu
wataanza kuelekea Dodoma Ijumaa ya leo ambapo tunaamini mpango huo utafanyika
kesho Jumamosi katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,” alisema.
Tukio
hilo linafanyika kwa mara ya kwanza ikiwa ni mpango wa kuwaweka sawa vijana kwa
ajili ya kuangalia namna gani ya kujiendeleza kimaisha kwa kutumia fursa
wanazokutana nazo.
No comments:
Post a Comment