MAMBO FULANI
MUHIMU
NI jambo la busara
mno kama wewe ni mpenzi wa safu hii kiasi cha kuwa na mimi kila Jumamosi kama
ya leo. Hakika, wewe unanifanya niendelee kuwapo hapa kuelimishana, kupeana
hili na lile katika suala zima la uhusiano wa kimaisha na mapenzi.
Uhusiano
Ndugu msomaji
wangu mpendwa, watu tunatofautiana sana katika kila kitu kwenye mambo ya
kimaisha. Katika suala hilo, wapo ambao wana mapungufu ya kila aina.
Kwa mfano, katika
uhusiano na maisha, kuna watu ambao suala la utundu katika mapenzi si asili
yao. Ni wazito kiasi cha kuwafanya wapenzi wao, wake au waume zao kukerwa nao.
Kwa bahati mbaya,
upungufu huo unageuka kuwa haki ya wenzao kuwasaliti kisa wanahitaji wasichana
au wavulana wepesi, watundu na wanaojua mambo ya mapenzi.
Si sahihi na jambo
hilo linatakiwa lipingwe kwa namna moja ama nyingine, maana kama kila asiyejua
mapenzi ana haki ya kuachwa, basi wataachwa wengi mno.
Wasiokuwa na uwezo
au utundu wa kuwatosheleza wenzao kwasababu hawajui mchezo huo ni wengi
kulingana na mahitaji ya jamii au wale waliokuwa kwenye uhusiano nao.
Kutokana na hilo,
unapokuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye umegundua kuwa hana uelewa kwenye suala
zima la mapenzi, hakika unapaswa kulichukulia jambo muhimu mno.
Usimuache eti
kwasababu hakutoshelezi au hufurahii lolote unapokuwa naye. Kinyume cha hapo,
jamii inapaswa ikulaumu, maana hadi kugundua kuwa uliyekuwa naye hakutoshelezi,
si mjuzi wa mapenzi, ina maana wewe ni hodari zaidi yake.
Kwa sababu hiyo,
jinsi ulivyokuwa wewe, unaweza kumfundisha mbinu nyepesi na rahisi kwa hatua ya
kwanza na baadaye mpenzi au mke wako atakuwa mwenye kukupa kile kinachostahili.
Dawa si kumuacha,
maana hata hao utakaokutana nao m bele ya safari wanaweza kuwa wazito zaidi ya
uliyokuwa naye awali. Utaacha wangapi? Je, kama wewe ndio hujui ukiachwa
utafurahi?
Nimekuwa nikipata
maswali ya kila aina kutoka kwa wasoamji wangu, huku mbinu gani, au malalamiko
ya watu wasiojua mapenzi kwenye uhusiano likichukua nafasi kubwa.
Kwa sababu hiyo,
kila mtu anapaswa kumfungia kazi aliyekuwa naye katika hali yaa kuhakikisha
lazima awe mjuzi. Nasema hivi maana si vibaya kumuelekeza mtu wako.
Na wale
wanaoelekezwa nao lazima wajuwe kuwa jambo hilo linatokana na wapenzi wao, wake
au waume zao kuhitaji kuwa nao kwa kipindi kirefu, hivyo wakubali kwa roho
moja.
Kuna wale ambao
wakifufundishwa au kuelekezwa kulingana na mahitaji ya watu wao, huwa wanyonge
au kulalamikika kuwa wamedharauliwa na watu wao.
Wengine hufika
mbali kwa kuanza kuwachukia watu wao, au kuwaona ni wahuni maana suala hilo
wamejifundishia wapi? “Niondolee uhuni wako, haya mambo wewe umeyajulia wapi,”?
ni kauli inayotoka katika baadhi ya vinywa vya watu wakiwaeleza wapenzi wao,
jambo linalozalisha kukata tamaa kwa wenzao.
Badala ya kusema
hayo, watu ambao hujitolea kuwaelekeza wapenzi wao, huwa na lengo la kuwaweka
katika nafasi nzuri, ili wajuwe namna ya kukabiriana na suala zima la uhusiano
wa kimapenzi.
Ingawa kweli wapo
watu ambao hawatosheki kiasi cha kutoka nje kila siku, lakini ni tofauti na
wale wanaotoka au kuwa na wengine kwasababu hawatoshelezwi na watu wao.
Wale
wasiotoshelezwa ni rahisi sana kutoka nje wakiangalia kuwa waliokuwa nao
majumbani mwao au kwenye uhusiano hawana mbinu za kuwatoa kijasho.
Ni jambo la
kujiuliza kwa kina. Je, mimi na wewe tunapokuwa kwenye mambo ya wakubwa wapenzi
wetu, wachumba wetu, wake au waume wanapokeaje uwepo wetu?
Je, wanafika
kileleni au ndio tumekuwa wazito, tukikimbia hatua moja tumechoka, hatutaki
kuendelea hivyo kuwaacha wenzetu katika hali mbaya kiasi cha kufikia kutamani
wengine?
Wehenga wamesema,
usipojenga ufa, basi utajenga ukuta.
Tukutane tena wiki
ijayo.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment