Na Mwandishi Wetu, Mtwara
Vita Mtwara yaendelea, mtaa wa
Mkanarendi wageuka uwanja wa vita
HALI inazidi kuwa mbaya mkoani
Mtwara, katika vuta nikuvute ya wananchi na askari polisi katika mvutano wa
gesi, huku nyumba 10 asubuhi hii mtaa wa Mkanarendi zikichomwa moto na kuzua
taharuki kubwa mjini hapa.
Hali ilivyokuwa mkoani Mtwara
Mtaa wa Mkanarendi ni ule
unaoishi wananchi wa kawaida, hivyo jeshi la polisi limejazana katika mtaa huu
kwa ajili ya kuendelea na harakati za kutuliza ghasia.
Handeni Kwetu Blog ilishuhudia
nyumba hizo zikichomwa moto na kuendeleza mvutano wa wananchi, ikiwa ni
mwendelezo wa tangu jana mchana baada ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati na
Madini, kusoma hutuba ya Bajeti yake.
Kwa kawaida, mvutano huo ni
mkubwa na ni hatari kubwa mjini hapa, huku vitu mbalimbali vya hatari
vikitumiwa na kuwawafanya wananchi wengi waishi kwa hofu katika majumba yao.
Hata hivyo haitoshi, baadhi ya
watu wasiokuwa waaminifu nao wameingia kazini kuendeleza kufanya uhalifu wa
aina mbalimbali, ikiwamo kuingia katika majumba ya watu na kuiba, hasa katika
maduka na maeneo mengine.
Jana, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, aligeuka mbogo kwa kuwataka wote
wanaondeleza kufanya ufedhuli huo wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali za
kisheria.
Kiini cha mgogoro huo ni
wananchi wa mkoani Mtwara kutaka serikali isisafirishe gesi yao iliyogunduliwa
mkoani kwao na kuipeleka jijini Dar es Salaam, badala yake shughuli zote
zifanyike mjini hapa, ikiwa ni njia ya kuundeleza mji huo.
Jana mitaa mbalimbali iliwaka
moto, ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto nyumba za serikali na baadhi ya madaraja
ambayo ndio kiini cha maendeleo katika mji huo ambao baadhi ya wananchi wanadai
umesahaulika.
No comments:
Post a Comment