https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, May 06, 2013

Mchezaji wa Chelsea amnanga vibaya mno Star wa Bongo Fleva Diamond


                        Adam Nditi kushoto na Diamond
Kwa msaada wa mitandao
MWANASOKA wa Tanzania, anayekipiga katika klabu ya Chelsea, kikosi cha pili, ambaye kwa sasa anaishi nchini Uingereza, Adam Nditi ameiponda show ya Diamond mjini Reading nchini humo na kudai ilikuwa ni aibu tupu na kusababisha kuwakera mashabiki.
 
Kijana huyo alionyesha kuchukizwa na shoo ya Diamond kwa kuandika kwenye mtandao wa twitter juu ya madudu ya msanii huyo mwenye jina kubwa Tanzania.

“Diamond jana manyago aibu tupu waswahili lazima tubadilike it’s
embarrassing,” ametweet.

“Hajafanya jambo lolote ila shoo ilikuwa haina very unprofessional
kwenye tangazo walisema inaanza saa 3 usiku jamaa amefika saa 1
asubuhi.”

“Jukwaa lilikuwa ovyo kama vile watu hawajalipa kumuuona mmoja
Wa wasani wanaotamba bongo nyimbo zilikuwa zinapigwa redioni
alikuwa haimbi.”

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...