Meneja Masoko wa kinywaji cha Chilly Willy kinacho sambazwa na kampuni ya
TSN Group, Yohana Manoli (Kushoto) akimkabidhi jezi mwenyekiti wa Taswa
FC, Majuto Omary (wa kwanza kulia) katika hafla fupi ya makabidhiano
iliyofanyika kwenye mgahawa wa Hadees. Kulia ni Meneja Uhusiano wa TSN Group,
Meshack Nzowah.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kinywaji maarufu cha kuongeza nguvu, Chilly Willy Energy Drink kimetoa
msaada wa jezi na mipira kwa timu ya soka ya waandishi wa habari za
michezo nchini, Taswa FC na timu ya Netiboli, Taswa Queens kwa ajili ya
kutumika michezo yake mbali mbali.
Meneja Masoko wa Kampuni ya TSN Group kinachosambaza kinywaji cha Chilly
Willy Yohana Manoli alikabidhi vifaa hivyo kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto
Omary katika hafla fupi iliyopfanyika kwenye mgahawa wa Hadees uliopo katikati
ya jiji la Dar es Salaam.
Manoli alisema kuwa sababu kubwa ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Taswa SC ni
kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kuendeleza michezo nchini na
hasa ukizingatia kuwa kinywaji cha Chilly Willy hakina kilevi na ni maalum kwa
wanamichezo.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TSN Group, Meshack Nzowah alisema
kuwa kinywaji chao cha Chilly Willy kina ubora wa kimataifa na wanaamini kuwa
wanamichezo na wanajamii wataanza kutumia kinywaji hicho katika shughuli
mbalimbali.
“Chilly Willy ni kinywaji ambacho hakina kilevi, kina ubora wa kimataifa
na kutokana na hilo, kampuni ya TSN Group ikaamua kukisambaza nchini kwa lengo
la kutoa bidhaa iliyobora zaidi, tunaamini wanamichezo wataanza kutumia hiki na
vile vile ni maalum kwa waandishi wa habari na wadau wengine nchini,” alisema
Nzowah.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza kampuni inayosambaza
kinywaji cha Chilly Willy na kuwaomba waandishi wa habari kuanza kutumia
kinywaji hicho. Majuto alisema kuwa Chilly Willy imetambua mchango wa
Taswa SC katika kuendeleza michezo na kutoa msaada huo.
“Ni faraja kubwa kuwa na kinywaji hiki hapa nchini na hasa kwa kutujali
wana habari, kwa vifaa hivi, Taswa FC na Taswa Queens zitakuwa na nguvu na
ubora kama wa Chilly Willy,” alisema Majuto.
Majuto alisema kuwa jezi hizo watazizindua rasmi Jumapili katika mechi
dhidi ya timu ya kombaini ya mabondia wa ngumi za kulipwa nchini itakayochezwa
kwenye uwanja wa Leaders Club kuanzania saa 5.00 asubuhi.
Alisema kuwa timu ya mabondia itaongozwa na bondia mkongwe nchini, Rashid
“Snake Man” Matumla na mabondia wakali wengine kama Francis “SMG” Cheka,
Cosmass Cheka, Mbwana Matumla, Karama Nyilawila, Maliki Kinyogoli, Hassan
Matumla, Daudi Mhunzi, Saidi Yazidu, Francis Miyeyusho , Thomas Mashali,
Charles Mashali na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment