Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Makubi Film Production and
Sports Promotions, juzi imetangaza kuendesha mashindano ya Uzalendo Cup yakiwa
na lengo la kuwawezesha vijana wanaocheza timu za mitaani kuonesha uwezo wao wa
kucheza soka, yakipangwa kuanza kutimua vumbi Mei 23.
Willson Makubi, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Willson Makubi, alisema kuwa pia mashindano hayo yatatumika
kuwatafutia wachezaji hawa timu kubwa zinazocheza ligi mbalimbali za kitaifa
hapa nchini.
Alisema kuwa mashindano hayo mashindano yatashirikisha jumla ya
timu ishirini kutoka kata za Makurumla, Mburahati, Manzese, Mabibo na Ubungo
zote za Mjini Dar es Salaam, ambapo zitatoa timu za kushiriki katika mashindano
hayo.
“Timu hizo ni zifuatazo ni pamoja na Mti
Pesa, Dago, Mburahati United, Pampona, Israel Academia, Mingo,Wazulu, Mabibo
Sokoni, Makutano, Midizini Market, Arizona, Mzozo, East Daz, Yakusela, Ranger, Umoja,
Darton, Uamsho, Kota Football Club na timu ya Wanafunzi wa Chuo cha Filamu (TFTC).
“Mashindano hayo yamezindulizwa juzi na Mkuu
wa kituo cha Polisi Magomeni, ASP Mwanne Salumu, ambapo katika mazungumzo yake,
aliziasa timu shiriki kuonyesha vipaji vyao halisi sambamba na burudani ya
mpira wa miguu,” alisema.
Mashindano hayo yanadhaminiwa na Redwood
Film Academia, Wendo FaceProduction, Global Publishers, Fleva Fm radio Dodoma.
No comments:
Post a Comment