Hii ni sehemu ya mwili iliyosalia kama inavyoonekana
Baadhi ya nguo alizokuwa nazo marehemu huyo ambae jina halijafahamika
Hiki ni kitenge ambacho alikuwa amevaa mwanamke huyo
Mashuhuda wa tukio hilo na askari kanzu wakitoka kuchukua mabaki ya mwili huo
Mabaki ya mwili wa mwanamke huyo yakihifadhiwa katika mfuko maaalum
Wananchi na polisi wakiupakia mwili huo katika gari la polisi mchana huu
Polisi
wakiuhifadhi mabaki ya mwili huo chumba cha maiti hospitali
ya rufaa ya mkoa wa Iringa
..............................................................................................................................................
Mabaki
ya mwili wa mwanamke mmoja ambae anakadiliwa kuwa na miaka
kati ya 25 hadi 30 imekutwa eneo la Magereza Kata ya
Miyomboni Kitanzini katika Manispaa ya Iringa leo.
Mabaki hayo
yamekutwa majira ya saa 6 mchana wa leo ikiwa imesambaratika
kutokana na kuoza imekutwa leo na maofisa wa magereza ambao
walikuwa katika eneo hilo na wafungwa wakikata miti kwa
ajili ya kuni na kukutana na mifupa hiyo.
Baadhi ya
mashuhuda walidai kuwa mwanamke huyo ambae alikuwa amevalia
suruali nyeusi ,kilemba cha kitenge chenye madoa makundu,njano
,meusi na meupe pamoja na skafu yenye rangi nyeupe na nyeusi huku
pembeni kukikutwa kitenge chake chenye rangi mchanganyiko kama
kilemba kwa maana ya makundu,njano ,meusi na meupe.
Hata
hivyo mashuhuda hao walisema kuwa mwanamke
huyo alipoteza maisha yake kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na
jinsi ulivyoharibika na kukauka kupita kiasi .
Mazingira ya
kifo cha mwanamke huyo yanaonyesha kuwa ni tata kutokana na
polisi waliofika eneo hilo kukiri kutokuwepo kwa
taarifa yoyote ya mtu kupotea na kuwa yawezekana alivamiwa
ama alikufa kwa matatizo yake ama alikuwa akitoka Hospitali.
Hata
hivyo eneo hilo ambalo mabaki hayo ya mwili yamekutwa ni eneo ambalo lipo
jirani zaidi na njia ya mkato inayotokea Ipogolo hivyo ilikuwa ni
rahisi zaidi watu kuuona mwili huo.
Mabaki ya
mwili huo yamechukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment