KATIKA
siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari hasa hasa kwenye mitandao ya
kijamii nchini kumekuwa na taarifa rasmi na zisizo rasmi kutoka kwa Mwanamuziki
Lady Jaydee alilalamikia Kituo chetu cha Clouds FM na wakurugenzi wake Ruge
Mutahaba na Joseph Kussaga.
Ruge Mutahaba akizungumzia mustakabali wa Made in Tanzania sambamba na sakata lao na Lady Jay Dee
Kwa
mtazamo wangu, kila mwananchi ana haki ya kutoa maoni yake ingawa kwenye nchi
yetu ya Tanzania, tumezoea maoni hayo kutolewa kwa lugha ya ustaraabu na staha.
Maoni
kuhusu nani wa kuja kwenye msiba wako au nyimbo za kupigwa kwenye msiba wako ni
haki ya kila mwananchi na hakuna atayeuingilia uamuzi huo. Maoni pia ya redio
gani mtu anaipenda au tv gani pia nayo ni utashi wa mtu mwenyewe.
Uongozi
wa Clouds FM ulikuwa umefikia maamuzi ya kutojadili jambo hili kutokana na
kuamini kuwa ni tatizo binafsi la mtu na sio jambo lenye maslahi ya Taifa hivyo
kwa uhalali linahitaji majadiliano au mazungumzo binafsi.
Sura
ambayo jambo hili limewekwa na kulifanya kama dharura ya kitaifa sio sahihi
kabisa kutokana na kukosekana na hoja za
kina za kuhitaji majibu na pili kukosekana kwa ujumla wa tija kwa tatizo hili
kitaifa.
Bado
ninaamini linatakiwa kubaki kama tatizo la mtu binafsi ila inapofika taarifa
zikapotoshwa kwa nia ya kuwapa mtazamo tofauti wasikilizaji wetu, Clouds FM
inataka kuweka maslahi ya wasikilizaji, wabia wetu wa biashara na watanzania
wote mbele kwa kuwapa taarifa sahihi za jambo hili.
Clouds
Media Group inapata lawama kubwa sana kutoka kwa watu wengi ambao pamoja na
kuunga mkono ukimya wetu wanajiuliza ni kwanini hatukufanya jitihada za
kumaliza tatizo hili bila kufika hatua iliyofikia sasa ya matusi, kebehi na
vitisho kutwa vinavyoelekezwa kwetu na pia vinaendelea kuichafua tasnia ya
muziki hasa hasa Bongo flava; ambayo imefika mahali inaonekana kila changamoto
inayomkabili msanii wa Bongo flava lazima itatuliwe kwa njia za mabavu (matusi,
vitisho na kuchafuana).
Lawama hizo sio za kweli na naomba nirudi nyuma
kidogo kwenye historia ya jambo hili. Tarehe 14 mwezi wa 12 mwaka 2012 kwenye
tweeter account ya Jaydee, alipost kifuatacho:
Nilichofanya
ni kumpigia simu na kuzungumza nae.
Akasema sijaandika kwenye blog chochote, nikamwambia Jide mi nakuheshimu
sana. Nimekupigia kwasababu naamini kama kuna kitu chochote ni bora nisikie
kwako, nategemea na wewe pia utanipigia iwapo kuna jambo lolote lile.
Tulikotoka
sisi hatutakiwi kuendeshwa na majungu na maneno ya mtaani.Hiyo ilikuwa tarehe
14 mwezi December mwaka jana. Baada ya kama dk 10 hivi akanitumia msg ( ambazo
bahati nzuri nilizihifadhi) na kusema ni kweli alikuwa ananizungumzia mimi kwa
sababu kuna vitu kadhaa vinamsumbua na aliambiwa mimi ndo nilihusika navyo.
La
kwanza, ‘nililipa matangazo ya shs laki mbili na 40 ila hayajachezwa na wala
sijarudishiwa hela yangu, nimeambiwa umekataza matangazo yangu ya Nyumbani
lounge yasipigwe’.
La
pili, naruhusu watangazaji wangu wamtukane ikiwa ni pamoja na kupromote zaidi
bendi ya Skylight.
Pamoja
na kwamba yeye alinitumia message, mimi nilimpigia simu na kumpa ufafanuzi wa
yote hayo niliyosema hapo juu.
Nikasema,
Biashara
yetu sisi ni matangazo…..kwanini tukataze matangazo yako yasipigwe?? Labda
bahati mbaya tu, jamaa anayebook matangazo alipitiwa kuyabook kibinadamu ila
Gadna si anakuja hapa kila wakati, kwann asimkumbushe tu?? Tutayasogeza tu
mbele hadi wiki inayofuata, kwanini niyakataze wakati muda sio mrefu tumetoka
kuleta biashara ya Repa bora wa bendi hapo hapo Nyumbani lounge.
Niliendelea
kujibu kuwa sio kweli kabisa, siwezi kuruhusu jambo kama hilo na kama ni kweli
mtangazaji anamtukana anifahamishe ni nani na kwenye kipindi gani, nitasikiliza
kipindi na kama ni kweli nitamfukuza kazi ( Clouds ina mitambo ya kuhifadhi
matangazo yake yote kwa takribani miezi 9).
Hili
nilimjibu kwa kirefu kidogo ikiwemo kumwambia akaze buti maana Skylight Band
wanakuja juu nk nk. (Skylight Band ni bendi inayofanya vizuri sana hapa mjini
na ilipoanza ilichukua baadhi ya majina makubwa kutoka Machozi Band).
Baada
ya kumaliza mazungumzo tuliagana vizuri tu kwa miadi ya kukutana nikirudi maana
nilikuwa safarini.
Kwahiyo
ukiniuliza Jaydee anacholalamika ni nini??? Jibu langu litakuwa ni hayo mambo
mawili maana hata nyie watanzania wenzangu mnaosoma mitandao ya kijamii
mtakubaliana na mimi kuwa amekuwa anashambulia personality zetu, mimi na
Mkurugenzi mwenzangu bila kuweka wazi hoja za msingi kuhusu yale anayotutuhumu
nayo.
Nimejitahidi
sana kuelewa tatizo lake hasa ni nini na imekuwa inanipa shida kidogo??
Nimejitahidi sana kufikiria ni mirija ipi ya biashara kwake imeingiliwa, nakosa
majibu???
Clouds
FM ni ya watu na watu wanaweza kufanya makosa kweli na hata kusababisha
matangazo ya laki 2 na 40 yasirushwe, kwa hilo nilishazungumza na Jaydee na
kuomba radhi toka tarehe 14 December 2012. Clouds FM haina ubia wowote ule na
Skylight Band (ni bendi iliyoanzishwa na Mtanzania)hivyo kuipromote ni katika
misingi ile ile ya biashara kama tunavyopromote bendi yeyote ile na vilevile
Clouds FM pia haihusiki kabisa na kutetereka kwa biashara ya chakula, vinywaji
na bendi inayofanyika Nyumbani lounge. Inashangaza hata kuhusishwa na biashara
ya Nyumbani lounge…!!!
Sina
ugomvi binafsi na Jaydee wala Gadna, na tarehe 12 February mwaka huu, nilienda
kuazima stools kwa ajili ya shooting kutoka kwenye sehemu yao ya biashara
ingawa yeye amekiri kuwa na ugomvi mkubwa na sisi binafsi na Clouds kama
chombo.
Nyimbo
yake iliyotoka ya Joto Hasira ilipokelewa vizuri sana kulinganisha na nyimbo
mbili zilizopita ‘Yeye’ na ‘Mimi ni mimi’ ambazo hazikufanya vizuri pamoja na
jitihada kubwa ya kuzipromote.
Joto
Hasira iliacha kupigwa kutokana na shinikizo lake mwenyewe, ikiwa imeshachezwa
mara 48 ndani ya wiki tatu toka imetoka wote tulipigwa na bumbuwazi na
kujiuliza ni kitu gani tumefanya kuambiwa hatupigi nyimbo na lawama nyingine.
Kama
ofisi tukaona tukae kimya na kusubiri hatua inayofuata ukizingatia tuliendea
kupiga nyimbo na video hata baada ya maneno makali ya mwanzo. Kauli
haikubadilika, mbaya zaidi kauli za kebehi na kuchafuana zikaongezeka hadi
kufikia uamuzi wa sisi kama taasisi kuamua rasmi kutopiga nyimbo zake hadi
atakapofuta kauli zake na kuomba msamaha.
Kupiga
au kutopiga nyimbo kwa kituo cha redio ni jambo la kawaida na kwasababu ni
chombo binafsi ni muhimu kwa watu kama Jaydee na wasanii wengine (na hata
wananchi wa kawaida) kuelewa kuwa kila ofisi ina taratibu zake na iwapo
utatokea ukiukaji wa taratibu hizo, policy ndo zinaongoza maamuzi.
Hebu
tujiulize, mbona sio mjadala wa Taifa msanii Diamond hapigwi karibu miezi sita
sasa kwenye station ya Magic FM, Ray C na Ali Kiba kwa karibu mwaka mzima
walikuwa nyimbo zao na video hazipigwi na East Africa hadi walipoomba msamaha,
hadi Yanga kwa muda mrefu walikuwa hawatangazwi habari zao kwenye chombo kimoja
cha habari. Hayo ni mambo ya ofisi binafsi na hakuna anayeweza kulaumu maamuzi
hayo.
‘Management
reserves the right of admission’……nani hajaona kibao hiki kwenye hoteli nyingi
tu nchini, nani asiyefahamu kuwa kuna hoteli ambazo ukienda kama mwanamke peke
yako unakataliwa?
Hizi ni taratibu na kila mahali zipo…..hata nyumbani lounge
ndo maana Sam Machozi ambaye yuko Skylight Band zamani alikuwa mwanamuziki wa
Machozi Band amepigwa marufuku pale Nyumbani lounge na halalamiki maana ni
sehemu binafsi na ina taratibu zake. Ni tofauti na sehemu za wazi za umma kama
Mnazi mmoja au kituo cha basi cha Magomeni.
Clouds
Media Group inafuata taratibu zote za nchi na za kimkoa ila na yenyewe pia
inaweka taratibu zake za uendeshaji. Sasa isifike mahali Clouds inapoweka
taratibu zake hizo na kuzitekeleza inaonekana inafanya makosa.
Yaani
hata tarehe za kufanya show nchi hii tunatakiwa kupeleka maombi sehemu ili watu
zaidi ya mmoja wasifanye show kweli???
Kwanini tunachanganya ushindani na fitina.
Acha
ziwepo bendi 10 zinazoshindana, kuanzishwa kwa bendi nyingine kusiangaliwe kama
fitna. Na hata mtu akianzisha bendi kwa
kuchukua wanamuziki kutoka kwenye bendi nyingine, si ndio dhana ya ushindani???
Kama
ni kulalamika kuanzishwa kwa bendi nyingine au kuchukuliwa wanamuziki, Dadaangu
Asha Baraka si angeshafanya maandamano nchi nzima. Ila wote tunatambua kuwa ni
jasiri ndo maana anatulia na kuanza upya.
Mbona
watu hawalalamiki baa zinapofunguliwa 10
mtaa mmoja, au saloon za nywele, moja jirani na nyingine. Ni lazima tukubali na
tuzoea ushindani.
Pamoja
na ushindani kingine ninachoomba
kuwasihi watanzania wenzangu hasa hasa wasanii wetu zaidi ni kuwa kila mtu na kila kitu kina ‘shelf
life’. Watu wa zamani naamini wanamkumbuka Power Mabula.
Alikuwa
anatisha sana wakati ule. Au nani anaweza kusahau umaarufu wa Mzee Nobert
Chenga na Kundi la Muungano cultural troupe au labda huko ni nyuma sana; nani
anamkumbuka Kanda Bongo Man, alicharge laki moja enzi hizooo….au labda hapa
katikati umaarufu wa Muumini, Mr Nice au mtu kama Saida Karoli (alijaza
Stadium).
Wote
hao walikuwa maarufu sana. Sasa wasanii hawa na wengine wanaokuja wasipojiandaa
kuelewa kuwa kila kitu kina muda wake, tutakuwa na taifa la vijana ambao
asubuhi mpaka jioni badala ya kuhangaikia fursa nyingi zilizopo wataishia
kutafuta mtu wa kumlaumu.
Ni
lazima Edibily Lunyamila atarithiwa sehemu yake na kina Mrisho Ngassa ambaye
naye muda utapita ni lazima atawaachia kina Simon Msuva. Wapo watu kama kina
Dully Sykes walioanza kujiandaa kwa kuwaachia kina Diamond na wao kufungua
studio na kuwa maproducer.
Suala la kupokezana vijiti halikwepeki kuanzia
makazini, mpirani na hata kwenye sanaa. Cha kufanya ni kujiandaa kwa maisha
yako baada ya kugawa kijiti chako.
Taarifa
za kutaka kuua muziki wa Bongo flava kwa makusudi zinashangaza, ili iweje sasa?
Clouds inategemea matangazo ya biashara kama asilimia 95 ya mrija wa mapato na
muziki tunaopiga redioni ni sehemu ya maudhui kwahiyo hakuna namna yeyote ile
tutataka muziki huo upotee. Tunafanya juhudi zote hizi kwasababu tunahitaji
nyimbo bora na wasanii bora ili tuweze kuendelea kuwa kituo bora cha redio.
No comments:
Post a Comment