Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman
Kinana, kwa kupitia wakili wake Eric S.Ng’maryo, wamemataka Mbunge wa Iringa
Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji
Peter Msigwa aombe radhi na kuifuta kashfa aliyoitoa dhidi ya Kinana kwa madai
kuwa anahusika na meli zilizokamatwa na meno ya tembo huku pia akiwa ni miongini
mwa mafisadi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
Kwa mujibu wa Tangazo lililochapishwa kwenye gazeti la kila
wiki, Raia Mwema la Jumatano, Mei 15,
Toleo namba 296, endapo Msigwa hatafuata masharti ya wakili Ng’amaryo ya
kumuomba radhi Kinana, basi atafunguliwa kesi itakayokuwa na madai makubwa na mengi, sambamba na
kubebeshwa mzigo mkubwa wa mamilioni ya shilingi.
Wakili huyo alielezea jinsi Msigwa alivyopotosha umma katika
mikutano yake ya kisiasa, sambamba na hutuba yake bungeni, akiwa kama Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mkutano wa Msigwa inadaiwa kuwa aliufanya Aprili 21, shule
ya Msingi Mbugani, wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, ambapo alizungumza mengi
ambayo yalisababisha usumbufu mkubwa na kuondoa hadhi ya Katibu huyo wa CCM,
Kinana.
Kutoa tangazo hilo na tamko rasmi la wakili wa Kinana ni
ishara kuwa moto wa kisiasa umezidi kupamba moto, huku watu wengi wakihusishwa
katika kashfa ya usafirishaji wa maliasili za Taifa, jambo linalopingwa na watu
wengi.
No comments:
Post a Comment