https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, May 18, 2013

Jamhuri Kihwelo Julio apiga mkwara mzito, asema kuna waamuzi walitaka kuhongwa ili waihujumu Simba



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
IKIWA ni saa chache kabla ya kuanza kwa pambano la Simba na Yanga, linalosubiriwa kupigwa saa kumi za jioni, kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo Julio, amesikika akilaumu kuwa kuna waamuzi walikuwa na mpango wa kuhongwa na mtoto wa kigogo serikalini.
 
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo Julio
Julio alikutwa maeneo ya jiji la Dar es Salaam akipiga kelele kuwa kuna uwezekano wa kuandaliwa hujuma ili kuifanya Yanga iweze kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo.

Tupo imara kweli kweli, lakini kuna baadhi ya waamuzi walikuwa na mpango wa kuhongwa fedha na mtoto wa kigogo mmoja anayetaka kuipa ushindi Yanga kwa faida zao, ila tumelijua hilo,” alisikika Julio bila kumtaja mwamuzi aliyekuwa na mpango wa kupewa fedha hizo.

Mechi ya Yanga na Simba imekuwa na upinzani wa hali ya juu huku kila kona kukikuwa na mwingiliano wa watu wakilizungumzia pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu Tanzania nzima.

Waandishi kutoka nchi za Afrika Mashariki wameingia kwa wingi Tanzania kushuhudia mechi hiyo ya watani wa jadi, huku Yanga wakiwa na kumbukumbu  ya kufungwa bao 5-0 mwaka jana.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...