Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Juma Ally Salim ‘Mzee
Kankaa’ aligongwa na gari wakati akifanya mazoezi ya kutembea kufuatia ugonjwa
wake wa kiharusi.
Tukio hilo lilitokea Aprili 21, mwaka huu maeneo ya
Kariakoo, Dar ambapo gari hilo aina ya Toyota Voxy lilitokea ghafla na kumgonga
kidogo na kumsababishia michubuko miguuni na kichwani.
Dereva wa gari hilo alifanya uungwana kwa kumpeleka katika
Kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo ndugu zake walitaarifiwa na kwenda
kumchukua.
“Mzee Kankaa alitoka nyumbani na kuwaaga kuwa anakwenda
kufanya matembezi. Walijua ni karibu, lakini baadaye tukasikia taarifa kuwa
amepata ajali na yupo Kituo cha Polisi Msimbazi,” alisema Abdul ambaye ni mtoto
wa Kankaa.
Kuangalia mzee kama huyu katangaza sana kazi ya sanaa ya Tanzana
lakini saizi hali yake sio nzuri au tunasubilia siku yaza msiba kuonesha
ufahari wa kutoa michango pamoja na kuuza sura. Wengi wamefanyiwa hivyo sasa tubadilike
Watanzania wenzangu.
No comments:
Post a Comment