TAARIFA
KWAVYOMBO VYA HABARI
Shirikisho
la Muziki Tanzania (Tanzania Music Federation) tunasikitika kutangaza kifo vya
msanii ALBERT MANGWEA kilichotokea Afrika
ya Kusini akiwa kwenye shughuli zake za kimuziki . Tunawapa pole Wazazi, ndugu,
jamaa na watanzania wote kwa kuondokewa na mwanamuziki huyo mkongwe wa kizazi
kipya, marehemu tutamkumbuka kwa mengi hasa msimamo aliounesha katika mambo
aliyoyaamini, Alikuwa ni mtu mwenye jitihada hata mauti ilipomkuta alikua
kwenye kujitafutia riziki.
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba
Marehemu
alitambulika sana katika tasnia ya muziki kupitia wimbo wa GETO LANGU TU na
baadae alirekodi nyimbo nyingi zilizopendwa na jamii ya watanzania.
Tunawaomba
watanzania wazidi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu, Shirikisho lenu
lipo imara na tunashiriki kikamilifu katika msiba huu tukishirikiana na wadau
mbali mbali.
Tunapenda
kuwatangazia kuwa Shughuli nzima ya mazishi ya mpendwa wetu ALBERT MANGWEA zitasimamiwa
na Familia ya Marehemu, Shirikisho la Muziki kupitia chama cha Muziki wa kizazi
kipya na wadau mbali mbali.
Kwa
sasa tunakamilisha taratibu zote za awali, maandalizi na ratiba mzima itatoka
baadae. Tulifanya kikao na kaka wa
marehemu (KENNETH MANGWEA) na kukubaliana kuwa msiba utakuwa MBEZI BEACH eneo
la GOIG kwa sasa tuna shirikiana vyema katika kukamilisha haya.
Kama
mambo yatakwenda sawa, ikiwa ni pamoja na kuuleta mwil.i wa marehemu tunatarajia
kuaga siku ya Jumamosi na baadae kusafirisha kwa shughuli ya Mazishi huko
Morogoro eneo la Kihonda nyumbani kwa mama yake mzazi MAMA DENISIA MANGWEA.
Tunaomba
tushirikiane sote kwa PAMOJA katika katika kipindi hiki kigumu.
Taarifa
zaidi tutawapatia baadae kadri itakavyo bidi.
Bwana
ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe.
Vile
vile tunampa pole mwanamuziki Mgaza Pembe (M TO THE P) na kuomba maombi ya
watanzania kumuombea mwanamuziki huyo
ambaye aliyekuwa Afrika Kusini na Marehemu. M TO THE P amelazwa Afrika
Kusini. Tunamuombea apone haraka.
Addo
November Mwasongwe
Raisi
Shirikisho la Muziki Tanzania
0713396367/0754396367
29th
May 2013.
No comments:
Post a Comment