Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI ha hatari imejitokeza katika msiba wa Ofisa Habari wa
Bunge, Ernest Zulu, baada ya jana usiku kutokea mvutano kutokana na upande
mmoja kalazimisha aende kuzikwa kwao Songea, huku watoto wakitaka azikwe jijini
Dar es Salaam.
Marehemu Ernest Zulu kulia enzi za uhai wake.
Kabla ya kifo chake, marehemu alitoa usia kuwa akifa basi
azikwe jijini Dar es Salaam alipozikwa motto wake wa kwanza, hata hivyo kaka wa
marehemu, Emmanuel Zulu, amekuja juu akitaka mdogo wake akazikwe nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa mama wa marehemu, Telesia Zulu, yeye ametakiwa
na daktari asisafiri safari ya mbali kutokana na kupata ajali kubwa hivi
karibuni.
Aidha mtoto wa kwanza wa marehemu, Phelemona alisema msiba
huo umekuwa na utata kwasababu ya ndugu wanaofosi baba yake akazikwe Songea.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila alilazimika
kufanya kikao cha masaa zaidi ya matatu na ndugu wa marehemu kujaribu kutafuta
namna ya kuweka sawa mambo hayo.
Zulu anatarajiwa kuwasili leo kutoka nje ya nchi alipokuwa
anasoma, ambapo msiba wake umedaiwa kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya
kichwa na kupelekea kufanyiwa upasuaji.
No comments:
Post a Comment