Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa
taarabu nchini, Khadija Kopa, ameongezwa katika utoaji burudani katika fainali
za Miss Ukonga 2013, zinazotarajiwa kufanyika Mei 25, katika Ukumbi wa Wenge
Club, jijini Dar es Salaam.
Khadija Kopa
Warembo hao kwa sasa
wanafanya mazoezi makali katika Ukumbi wa Hill Tech, Ukonga, huku wakijifua
vilivyo kuhakikisha nao wanatoa burudani za aina yake katika usiku huo wa Redds
Miss Ukonga.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Mratibu wa shindano hilo, Chiku Chambuso, alisema kuwa
maandalizi ya shindano hilo yanaendelea, ikiwa ni kumalizana na mwimbaji huyo
wa taarabu, atakayeshirikiana kwa pamoja na Banana Zoro na bendi yake ya
B-Bendi.
Alisema kuwa anaamini
kuwa burudani za mwimbaji huyo wa taarabu na wengineo watafanya mambo makubwa
katika shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wao.
“Kutakuwa na burudani
za aina yake katika shindano hili ambalo mabinti wenye uwezo wa kucheza na
jukwaa wanajifua vilivyo katika kuhakikisha kuwa mambo yao yanakuwa mazuri.
“Naamini kila kitu
kitakuwa sawa katika kuhakikisha kuwa mabinti wanafanya mambo makubwa kwenye
shindano letu la Miss Ukonga 2013 lenye ushindani wa kila aina,” alisema.
Wadhamini wa
shindano hilo ni Redds, Z-Entertainment, UEFA go Pub, Break Point, Salut 5,
Mamushka Bar, Hilltech resolt, Kiota Jungle, Business Times, Times FM na Clouds
FM.
No comments:
Post a Comment