Mbunge wa Jimbo la Kigoma
Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa Muziki hapa
chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini hiyo iliyohusu
na harakati
rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema
leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa
Dodoma.kutakuwepo
na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya
uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi
mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa. Aidha pia mchana
huu kutakuwepo na burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za
kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania katika
uwanja wa jamhuri .
Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Patrick Ngowi kutoka kampuni ya Helvetic Solar Contractors, akizungumzia
fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ujasiliamali na pia alielezea ni
namna gani amefanikiwa mpaka kufikia kumilimiki lampuni yake binafsi
kupitia fursa alizokuwa akikumna na nazo na kuzifanyia kazi vilivyo.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo
akiuliza swali kwa Mh Zitto Kabwa kuhusiana na mambo mbalimbali ya
ujasiliamali na namna ya kuzitumia fursa hizo katika kujikwamua
kimaisha.
Mh Zitto kabwe akimsikiliza mmoja
wa washiriki wa semina hiyo alipokuwa akiulizwa kuhusiana na suala la
fursa zinazopatikana kwa vijana na namna ya kuzitumia katika ujumla wa
kujikwamua na ugumu maisha,ambapo watanzania wengi wamekuwa
wakizilalamikia.
Mtangazaji wa clouds FM kupitia
kipindi cha Power Breakfast-Gerald Hando akiikaribisha Meza kuu pamoja
na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa
Clouds Media Group unaokwenda sambamba na ujumbe wao thabiti kabisa
ulioitwa MADE IN TANZANIA,ikiwa na hamasa kubwa ya kuleta msingi
wa fursa kwa watanzania, msukumo ikiwa ni kuwashawishi watanzania
kuanza kuzifanyia kazi fursa hizi kwa umoja na maendeleo ambapo
TWENZETU, inakuwa neno rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi
kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita
dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na
wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa ikiwemo
semina ya fursa kwa watanzania,burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za
kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania
zitapatikana uwanja wa jamhuri mapema leo mchana.
Mmoja wa wasemaji kwenye semina
hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Zenno Ngowi kutoka kampuni ya
Tanzania Home Expo akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya
ardhi,ujenzi,na mengineyo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali
waliohudhuria kwenye semina hiyo leo mjini Dodoma.
Mmoja wa wasanii mahiri wa
Mashairi,Mrisho Mpoto akifafanua jambo kuhusiana na mambo mbalimbali
katika suala zima la wasanii kujipa nafasi ya Fursa mbalimbali
zinazojitokeza mbele yao na namna ya kuzifanyia kazi na kuziboresha
zaidi.
Mhe Zitto Kabwe akiwasili kwenye semina hiyo mapema leo,ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wasemaji wa semina hiyo.
Pichani ni washiriki wa semina hiyo kutoka sehemu mbalimbali mjini Dodoma leo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia
jambo kwenye semena iliyokuwa ikiendelea mapem leo kwenye hoteli ya
African Dreamz,nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Mtangazaji wa Clouds FM,Loveness Love a.k.a Diva akijitambulisha kwenye semina hiyo
Mtangazaji wa Clouds FM,Shaffih Dauda akijitambulisha kwenye semina hiyo.
wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo iliyoibua changamoto nyingi.
Kutoka Clouds FM,Millard Ayo,Dina Marios pamoja na Zamarad wakifuatilia jambo
Mtangazaji wa Clouds FM,Arnold Kayanda Diva akijitambulisha mbele ya washiriki waliofika kwenye semina hiyo.
Baadhi ya wasanii wakiwa ndani ya semina hiyo katika harakati
rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi zao,ambapo matembezi ya hisani
yamepangwa kufanyika kesho na Waziri Mkuu Mh.Pinda anatarajiwa kuyapokea
matembezi hayo.
Msanii Afande Sele na Msanii mwenzake wakiwa ndani ya semina hiyo wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa.
Mtangazaji wa Kipindi cha jahazi,Mussa Hussein akijitambulisha.
Mtangazaji wa Clouds FM,B Dozen akijitambulisha
Mbwiga Mbwiguke nae kama kawa akijitambulisha kwa washiriki wa semina hiyo.
Zamarad Mketena akijitambulisha pia.
No comments:
Post a Comment