Madaktari wakiwa kazini kuhakikisha wanaokoa maisha ya mtoto
huyo.
Inasikitisha sana kwa
mtoto wa miaka minne kufanyiwa kitendo kibaya na baba yake mzazi
Majukumu ya kuokoa maisha ya mtoto huyo yakisonga kwa kasi.
Afande Bwire akiwa na pingu zake wodini
Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama
mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa
kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa
kimapenzi.Endelea kupitia mtandao huu ili upate habar zaidi.Tukio hilo
limetokea jana jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake
Happiness (28) Elias huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu
kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.
Kwa mujibu wa
majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda
walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na
kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.
Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto,
majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na
baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya
sehemu za kichwani.Majirani kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari
polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi
la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.
Hata hivyo Wakati gari la Polisi likiwa katika mwendo wa
kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia
kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.
Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika
hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi
mkali wa polisi.
No comments:
Post a Comment