https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, May 12, 2013

Serikali mkoani Kagera huenda ikatumia JWTZ kuwasaka na kuwatia mbaroni watu wanaojihusisha na ujambazi wa kuteka magari.

Kanali Fabian Masawe akizungumza na wananchi.

Kanali Masawe alisema haridhiki na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi wilayani humo kwani wamekuwa wakikaidi amri ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa ya kusindikiza Magari ya mizigo na Abiria katika barabara hiyo na watu kuendelea kutekwa kwa kunyanganywa mali zao au kuuwawa na majambazi wa eneo hilo.


Alisema kitendo cha kukuta magari yakisafiri bila askari katika barabara yenye uhatari kiusalama ni kuonyesha dalili za Askali kushirikiana na majambazi kuhatarisha amani kwa wananchi wa wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.

Nobert Mahala,OCD Biharamulo

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Biharamulo,Bw.Richard Mbeho alisema kuwaalisha toa maagizo kwa Jeshi la Polisi wilayani Biharamulo kuhakikisha linawatuma askali katika barabara hiyo lakini utekelezaji wa maagizo yake unapuuzwa na watendaji hao ambao jukumu lao ni kulinda usalama wa raia na mali zao.

Hata hivyo Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Biharamulo ,Bw.Nobert Mahala  alijitetea kwa kusema kuwa jukumu la kusindikiza magari liko kwa Afisa Operation wa Mkoa ambapo majibu hayo yalimpelekea Mkuu wa Mkoa ,Kanali Masawe kusema kuwa kama  Afisa huyo  ameshindwa wajibu wake,asimamishwe kazi mara moja.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...