Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MBUNGE wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), ambape pia ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’,
amevunja rasmi uswahiba na Clouds FM, baada ya kuhoji uhalali wa serikali
kukubali kushiriki kwenye Made in Tanzania, mjini Dodoma, wakati wao ndio walalamikiwa na wasanii Tanzania.
Siku Sugu alipopatanishwa na Ruge Mutahaba. Kulia ni Tundu Lissu na kushoto ni Emmanuel Nchimbi.
Lady Jay Dee, Komando a.k.a ANACONDA
Maneno ya Sugu yaliambatana na kumsifia kwa kiasi kikubwa
mwanadada Judith Wambura, maarufu kama Lady Jay Dee ambaye kwa sasa yupo kwenye
vita ya maneno na mabosi wa Clouds FM, akiwamo Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.
Akizungumza leo mjini Dodoma, Sugu alisema kuwa kitendo cha
Waziri Mkuu Mizengo Pinda kushiriki kwenye Made in Tanzania, mjini Dodoma na
watu wanaolalamikiwa, ni kitendo kisichokubalika, hivyo kuna haja ya watu
kujiangalia upya.
“Hii haiwezi kukubalika hata mara moja, maana serikali
inapenda kukurupuka katika mambo mengi, yakiwamo haya ya malalamiko ya wasanii
yanayofanywa kila siku,” alisema.
Aidha, Sugu alimaliza hutuba yake kwa kumpongeza Lady Jay
Dee na kumtaka aongeze bidii katika kazi zake, hasa shoo yake anayotarajia
kuifanya mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa maneno ya Sugu leo mjini Dodoma, kuna kila dalili za kuibua upya bifu lake na Kampuni ya Clouds, ambayo ugomvi wao ulifikia tamati mwaka jana kwa kusuluhishwa.
No comments:
Post a Comment