Hii ndio barabara
kuu inayotoka Kilombero kuelekea lfaraka,Mahenge na Ulanga,eneo hili limekuwa
kero kubwa kwa wasafiri wanaotumia barabra hiyo, huku wananchi wakitumia barabara kuu ya Kilombero, kuelekea maeneo ya lfaraka, Mahenge, na
Ulanga, wakiilalamikia serikali ya wilaya ya kilombero kwa kushindwa kukarabati
shimo kubwa lililopo barabara kuu ya Kilombero-lfaraka na kusababsiha
adha kubwa kwa wananchi ambao magari yao hukwama kwenye shimo hilo na kusababisha
kulala hapo usiku kucha.
Shimo hilo klubwa
lililojaa maji kufuatia mvua zinazoendela kunyesha lipo kwenye barabara hiyo
eneo la Kidatu kilometa chache kitoka Kilombero mjini
Baadhi ya wananchi waliohojiwa na audifacejackson blog
walidai kwamba shimo hilo ni la muda mrefu na kwamba viongozi mbali mbali
wanapita eneo hilo na kushuhudia bila kuchukuha hatua yoyote.
"Bila huyu jamaa
mwenye trekta sijua hali ingekuaje,hata hivyo jamaa huyu anafanya kazi hii kwa
muda wa mchana tu ikifika jioni anaondoka zake, jana usiku kuna abiria wa basi
moja walipofika hapa wamekwama na dereva alifanya jitohadi kulivusha gari lake
bila mafaniki nakuradhimika kulala hapa huku baadhi ya abiria waliokuwa na
watoto wadogo wakilalamika watoto zao kung’atwa na Mbu na kupigwa na
baridi usiku kucha hadi alfaji trekta lilipofika na kulivuta
basi hilo, wananchi tutavumilia lakini iko siku uvumilivu utafika
kikomo”alisema Bw Abdalaman Ismail ambaye alikuwepo eneo la tukio alishuhudia ndugu
zake wakitaabika kwenye eneo hilo.
Trekta
ambalo linafanya kazi ya kuyafuta magari yanayokwama kwenye shimo
hilo,likifuta roli huku mataili yote manne yakiwa juu kufuatia roli hilo
kuwa na mzigo mzito
Basi hili likijitoa kutumbukia kwenye shimo hilo
Wananachi wakieleke kwenye basi lao ambalo lilikwama eneo hilo kwa muda mrefu,na kufanikiwa kuvutwa na trekta hiyo
No comments:
Post a Comment