Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UKUMBI wa
Hobours Club, uliopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger
Tenga anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi ya makocha wa ngazi
ya pili (Intermediate) itakayofanyika Jumatatu (Juni 3, 2013) kwenye
Mkurugenzi wa Ufundi Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA), Joseph Kanakamfumu, alisema Rais Tenga atakuwa mgeni rasmi
katika ufunguzi wa kozi hiyo itakayohusisha amakocha 26.
Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Alisema kozi hiyo itakayomalizika Juni 28 itakuwa imewezesha
kupatikana makocha watakaosaidia maendeleo ya mchezo huo katika Mkoa wa Dar es
Salaam na Taifa kwa ujumla.
Aliwataja makocha wa kozi hiyo kuwa ni Shadrack Nsajigwa,
Benard Mwalala, Steven Nyenge, Jemedari Said Kazumari, Zubeiri Katwila, Ibrahim
Masoud ‘Maestro’, David William Ngaga, Idd Abushir Mwinchumu, Rajab Mohamed
Nakuchema, Lubigisa Madata, Bakari Mahad, Greyson Swai, Chiwanga A.
Chiwanga, Sizza Mapunda na Muhibu Kanu.
Wengine
ni Omari Mbarouk, Omari Mohamed, Samuel Galafawo, Abdallah Mbogolo, Hassan
Msonzo, Akida Said, Emanuel Gabriel, Barton Msengi, Edgar Method Katembo, Elly
Kaiza na Renatus Benard.
Kozi
hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia kwa uongozi mpya wa chama
hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti Almas Kassongo.
Wengine walioingia madarakani katika uchaguzi huo
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mbezi Garden ni Meba Ramadhan (Makamu
Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa
TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu), Ally Hobe (Mhazini) na Wajumbe wa
Kamati ya Utendaji Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari Mapande.
No comments:
Post a Comment