TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA
UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI
JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013
Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho
nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa
juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika
kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013
na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.
Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya
watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko
wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa
bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda
mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa
Olasiti.
Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za
falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato
katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi
wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali
polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa
Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)
Rai hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili
ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen.
Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala
jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini
Arusha.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha
taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la
mlipuko wa bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika
katika shambulio hilo.
Baada ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya
mwanasheria mkuu wa serikali Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa
watuhumiwa hao wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona
kama kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati
walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Pia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka
dhidi ya victor S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za
mauaji na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea
kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenya na Uganda ambao tunashirikiana nao katika
upelelezi wa shauri hilo.
Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko
wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao
kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha,
4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya
taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao
zinaendelea kuimarika.
Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za
watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na
kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au
raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi
nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha
taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono
ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa
kukamatwa kwa watu hao.
ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.
No comments:
Post a Comment