https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, August 23, 2013

Wanafunzi wailalamikia shule ya Kwamatuku Sekondari iliyopo wilayani Handeni, mkoani Tanga



Na Rahimu Kambi, Handeni
BAADHI ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondary ya Kwamatuku, iliyopo Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, wameilalamikia shule yao kwa madai kuwa hawafundishwi kama inavyostahili, hivyo kuhofia matokeo ya 'ziro' kuendelea kushika kasi kila mwaka.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi hao walisema ufundishaji kwenye shule yao sio mzuri, hivyo matokeo kwenye ya ufaulu utaendelea kuwa ndoto.

“Hapa hakuna mwelekeo wowote, maana tunafundishwa kwa kiasi kidogo mno na mara zote hatuambulii chochote cha maana hali itakayotuweka sawa kwenye mitihahani yetu.

“Tunaomba serikali kwa kupitia Mkuu wa wilaya Handeni, sambamba na wataalamu wa elimu hasa Afisa Elimu wa Sekondari wilayani hapa kuliangalia suala hili kwa kina,” alisema.

Wanafunzi hao walitolea mfano mwalimu wa anayefundisha somo la Kingereza kutowajibika ipasavyo kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi hao jambo linalowafanya wafeli katika mtihani wa Taifa kila mwaka.

Akizungumzia tuhuma hizo, Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Kata ya Kwamatuku, Godfrey Bendera, alisema madai hayo hayana ukweli na yametolewa kwa sababu wanazojua wenyewe.

“Shule yetu ina bodi na ina uongozi mzuri, hivyo inashangaza kwanini masuala hayo yasiibuke kwanza kwetu na kuanzia katika ngazi za habari na kuibua maswali.

“Kwanza mimi sio msemaji wa shule hii, lakini katika suala hilo nabaki nashangaa na kujiuliza maswali lukuki, ukizingatia kuwa katika shule yetu utaratibu ni mzuri mno,” alisema Bendera.

Shule ya Kwamatuku, inatumiwa na vijiji vya Komsala, Kweingoma, Nkhale, Kwamatuku na wengineo, ikiwa ni kati ya zile zilizojengwa kwa wingi katika Taifa hili ili zitowe fursa ya kuwapatia elimu ya sekondari Watanzania.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...