NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Aggrey Mwanri, amewataka wazabuni kujenga miradi ya maendeleo mkatika Halmasahauri
nchini kwa kufuata masharti na weledi wao badala ya kuzigeuza Halmashauri hizo kama
shamba la bibi kwa kuchota fedha na kutekeleza miradi chini ya kiwango.
Naibu Aggrey Mwanri, pichani.
Hayo yamesemwa na Mwanri baada ya kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa
wodi ya kina mama wajawazito katika kituo cha afya cha Mkata inayosimamiwa na Kampuni
ya Elcat Builders (T) Ltd hapo jana, katika ziara yake wilayani Handeni mkoani
Tanga.
Alisema ni kawaida kwa wa kandarasi wanaopewa zabuni za usimamizi wa
miradi kutotekeleza kwa kiwango kinachostahiki huku wakipoteza raslimali fedha ya
serikali ambayo bila ya kuionea huruma nchi yao.
“Nakerwa nakitendo
cha wakandarasi kuzifanya Halmashauri kama shamba la bibi la kuchuma fedha na kutekeleza
miradi ya madudu, Mwenyekiti wa Halmashauri liangalieni hili na ikibidi muingile
kati ili kuhakikisha mnazisimamia kwa ukaribu fedha za miradi zinazotolewa naserikali,”alisema
Naibu Waziri
Naibu Waziri
alionyesha kukerwa zaidi baada ya kusomewa taarifa na mkandarasi wa Wilaya kuwa
mradi huo nia hadi ya Rais Kikwete aliyoitoa wa kati wa kampeni za urais nakuahidi
kutoa fedha kiasi cha Sh 100 kwa ajili ya utekelezaji ahadi ambayo aliikamilisha.
Injinia
Richard Mocha alisema kutoka namkandarasi huyo kuchelewesha ujenzi wa mradi huo
ndipo walipo muandikia barua ya kusudia la kusitisha mkataba kutokana kupitisha
muda wakukabidhi mradi huku jingo likiwa katika hatua za kupauwa.
“Mheshimiwa
Naibu Waziri ujenzi wa mradi huu mpaka utakapokamilika utagharimu kiasi cha Sh
Mil 96 huku kiasi kilichotolewa na Rais Jakaya Kikwete kiki wa nish Mil 100 na mpaka
hatua iliyofikiwa ya ujenzi ni sh Mil 10 huku ujenzi ukiwa bado unaendelea.
Hata hivyo Naibu waziri alisema siku mia moja ilizopewa kampuni yao
ya kuvunja mkataba alishauri zitakapokwisha mradi huo apewe mkandarasi mwingine
ilijengo hilo likamilike kwa wakati na wananchi waweze kupatiwa huduma kwa haraka.
No comments:
Post a Comment