Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAMASHA
linalojulikana kama Cheza Kidansi (CK) lililofanyika juzi katika Ukumbi wa
Vijana Social Hall, Kinondoni na kudhaminiwa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Mchumi wa Kata ya Makumbusho, jijini Dar es Salaam, Yusuphed Mhandeni,
lilikuwa la aina yake kwa kuhudhuriwa na watu wengi, bila kusahau bendi tatu
kubwa kufanya shoo ya aina yake.
Vijana wa Diamond Sound Original wakiwajibika jukwaani.
Cheza Kidansi
lilimualika Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, huku bendi
zilizotumbuiza katika tukio hilo la kusherehekea mwaka mmoja ni Victoria Sound,
Mapacha Watatu na Diamond Sound Original.
Akizungumza katika
burudani hizo zilizokuwa na lengo la kuhamasisha na kukuza muziki a dansi Tanzania,
Mhandeni alisema kwamba lengo lao ni kuona muziki unarudi juu kwa kasi kama
ilivyokuwa awali.
Alisema muziki wa
dansi una historia kubwa kwa Taifa la Tanzania, hivyo ni jukumu la kila mmoja
kuhakikisha kuwa dansi inarudi juu naa kufanya vyema katika tasnia ya muziki
huo.
“Nimehamasika sana na
muunganiko huu wa vijana wa Cheza Kidansi walioanzia katika mitandao ya kijamii
face book na baadaye kuona wakutane ili wajuane na kuzungumza jambo moja la
muziki wa dansi.
“Nashukuru kwa kila
mmoja wake kuhamasika pamoja na bendi zote zilizokubali kuja kujumuika na
vijana hawa, ukizingatia kuwa ndio sababu ya kuwapo katika tukio hili la aina
yake,” alisema Mhandeni.
Naye Mnyonge
alisema ni wajibu wa kila mmoja wao, wakiwamo viongozi wa serikali kuzialika bendi
katika matukio yao ili kuwaongezea kipato, badala ya kuelemea kwenye muziki wa
kizazi kipya.
Mbali na kuwa
mdhamini wa tukio hilo la Cheza Kidansi, Mhandeni pia ndio mlezi wa muunganiko
huo wenye lengo la kutafuta nguvu ya kuurudisha juu muziki wa dansi unaolekea
kushuka siku hadi siku.
No comments:
Post a Comment