Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
USAJILI wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu
(2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3
mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Uamuzi wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata
disc ya usajili msimu huu ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki
unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo
hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili.
Kutokana na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha
pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6 na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na
Hadhi za Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia
uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka
huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya
Vodacom msimu huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa
hazijajaza nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa
kuanzia Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.
Pia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha
usajili wao zinatakiwa kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya
mazoezi, nakala za bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo
yameelezwa kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom
No comments:
Post a Comment