Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANACHAMA wa Kikundi
cha Waandishi wa habari wanaojihusisha na ujasiriamali (Habari Group), wametoa
msaada wa vyakula na nguo wenye thamani ya sh. milioni moja kwa vituo viwili
vya kulelea watoto yatima kwa ajili ya sikukuu ya Idd El Fitri.
January Makamba, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia
Msaada
huo uliofadhiliwa na wadau mbalimbali ulikabidhiwa juzi, na wanakikundi hao
ikiwa ni njia ya kuonyesha ushiriki wao katika masuala ya jamii.
Vituo
vilivyokabidhiwa msaada huo ni Kituo cha Kulelea watoto yatima cha
Tahfidhil-Qur-An Al-Hidaya kilichopo Buguruni na kituo cha Al Furqaan Islamic
kilichopo Chanika.
Mweka
hazina wa Habari Group, Hellen Mlacky alisema kuwa msaada huo umechangiwa na
wadau mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
January Makamba, Mwenyekiti wa Aisha Sururu Foundation, Aisha Sururu, Waziri wa
Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Katibu Mkuu wa
Taasisi ya Mashekh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania,Sheikh Hamis Mattaka.
Wengine
ni mmiliki wa wa maduka ya Silva Boutique Madam Nora na Mkurugenzi wa kampuni
ya Quality Printers and stationaries,Amani sokko.
Alitaja misaada hiyo kuwa ni pamoja na nguo, sukari, mchele, maharage pamoja na mafuta ya kupikia.
“Sisi
kama wanahabari wajasiriamali kikundi chetu ni cha kusaidiana na hivyo tumeona
ni vyemka na sisi tukashiriki katika kuwasaidia watoto hawa ili nao
washerehekee sikukuu kama watoto wengine wanaoishi na familia na jamaa zao,”
alisema.
Akishukuru
kwa msaada huo, Katibu wa kituo cha Tahfidhil-Qur-An Al-Hidaya, Abubakar Simba
aliiomba jamii kuendelea kukisaidia kituo hicho ili watoto wanaolelewa waweze
kupatiwa mahitaji yote muhimu.
Kwa
upande wake Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Al Furqaan Islamic, Hamis Omari
alishukuru kwa msaada huo na kuitaka jamii kuwaona watoto hao ni sehemu yao na
kuwasaidia ili nao waweze kufanikiwa katika maisha yao.
No comments:
Post a Comment